Header Ads

WATENDAJI WA KATA MANISPAA YA MOROGORO WAPATA MAFUNZO MFUMO JUMUISHI WA UHASIBU NA UTOAJI WA TAARIFAZA (FFARS).

WATENDAJI wa Manispaa ya Morogoro wamepata mafunzo ya  Mfumo jumuishi wa Uhasibu na Utoaji wa Taarifa (FFARS) ambao umetayarishwa ili kukidhi mahitaji ya stadi sahihi (zilizoboreshwa) za udhibiti wa fedha katika ngazi za Kata.

Mafunzo hayo yamefanyika Ukumbi wa DDC Mbaraka Mwinshehe Manispaa ya Morogoro Septemba 11/2023.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mussa Mshana kutoka Ofisi ya Uhasibu Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa “FFARS”itatoa taarifa kuhusiana na jinsi ambavyo kanuni na taratibu za manunuzi zinavyozingatiwa, na pia kuwezesha utoaji wa taarifa kamili na za mara kwa mara za mapato na matumizi kwenda Halmashauri kupitia Kata.

Mshana amesema kuwa “FFARS” inajumuisha aina zote mbili za mifumo yaani mfumo wa “Manual” na wa ki-elektroniki.

Aidha, Mshana amesema , lengo kuu la kutumia "FFARS" ni kutoa uelewa mpana, maarifa na stadi za kuwezesha utendaji wa moja kwa moja kwa watumishi waliochaguliwa kutoka kwenye vituo kuhusiana na uhasibu na utoaji wa taarifa katika ngazi ya kutolea huduma pamoja na kuwawezesha washiriki kupata stadi za utunzaji vitabu muhimu vya uhasibu na kumbukumbu zingine za kifedha, na utayarishaji wa taarifa za fedha kwa vipindi mbalimbali

Kwa upande wa Mkufunzi mwengine kutoka Ofisi ya Uhasibu Manispaa ya Morogoro ,  Albert Hoja, amesema kuwa mwongozo huu wa mafunzo unatarajiwa kufikia madhumuni kama vile kuonesha mfumo na michakato inayotengeneza “FFARS”, kutoa nyenzo zitakazotumika kwenye mafunzo ya watumishi kutoka kwenye vituo yatakayo wezesha uelewa na utumiaji wa “FFARS” katika sehemu zao za kazi pamoja na  Kutumika kama rejea wakati wa utendaji katika sehemu za kazi.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.