Header Ads

WANANCHI MAFIGA WAPINGA OMBI LA CHUO KIKUU SUA KUTAKA KUMILIKI SHULE YA SEKONDARI MAFIGA.









 

WANANCHI wa Kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro wamekataa ombi la Chuo Kikuu SUA juu ya kutaka kumiliki Shule hiyo.

Kauli hiyo ya Wananchi wameitoa Septemba 09/2023 katika kikao Cha Wananchi Cha kujadili suala hilo kilichoongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Thomas Butabile.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti , Wananchi hao wamesema kuwa suala la ombi la umiliki Shule hiyo haliwezekani huku wakiwataka SUA kutafuta njia nyengine ya kupata Shule ambayo wanataka kuitumia kwa ajili ya Mafunzo.

wakifunga kikao hicho, Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe Thomas Butabile, amesema maoni yao wameyapokea na watayafikisha kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Kama barua ilivyotaka Uongozi wa Kata kujadili na kumshauri juu ya ombi hilo.

Chuo Cha SUA kimeomba kumiliki Shule hiyo  kufuatia vigezo vya wao kutoa ardhi kwa Manispaa ya Morogoro kuruhusu ardhi yao kujenga Shule 4  za Sekondari ikiwamo Mafiga, Bondwa , SUA  na Mbuyuni Moderm na Shule ya Msingi Chief Albert Luthuli.

Aidha, katika ombi la Chuo cha SUA kumiliki Shule hiyo, waliambiwa na Wizara ili Shule hiyo iweze kubadilishwa umiliki wanatakiwa kuwasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ili kibali Cha kumilikishwa kiweze kutolewa.

Kufuatia kauli ya Wizara ya kumuomba Mkurugenzi umiliki, Menejimenti ya Manispaa iliamuru suala Hilo lifike kwa Uongozi wa Kata ya Mafiga ili walitolee maamuzi na kumshauri Mkurugenzi wa Manispaa Kwa kushirikisha vikao vyote muhimu katika kupitia na kutoa mapendekezo ya suala Hilo.

Chuo Cha SUA kinaomba umiliki ili kutumia miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuitumia kufundisha mikondo ya Elimu ya JUMLA na mkondo wa amali.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media...

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.