Header Ads

DIWANI BUSORO ALETA KICHEKO SHULE YA SEKONDARI BUGURUNI MOTO



DIWANI wa Kata ya Buguruni Manispaa ya Ilala, Mhe. Busoro Pazi, amehakikisha shule hiyo uwepo wa Shelfu za kuhifadhia vitabu ili vitabu hivyo viwe katika utunzaji mzuri pamoja na meza za maktaba.

Busoro, amesema Shule hiyo ilikuwa na changamoto ya  shelfu na meza za maktaba  hivyo kwa kushirikiana na  wadau wake wa maendeleo wameona watumie nafasi hiyo kutengeneza shelfu hizo pamoja na meza za maktaba  ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki.

"Nimefanya ziara shule hii ya Sekondari Buguruni Moto  kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya  kazi ya utengenezaji wa shelfu za kuwekea vitabu pamoja na meza za maktaba shuleni hapo, kwa namna ya pekee nimshukuru Mdau wa Elimu Ndg, Vincent Daudi kwa kulifanikisha hili kupitia marafiki zake Elder na  Sister Low raia wa Marekani waliyojitolea fedha zao kwa kazi hiyo" Amesema Busoro.

Diwani huyo katika utendaji wake wa kazi amekuwa akitumia kauli mbiu yake isemayo Maneno kidogo Kazi zaidi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.chombohurumedia .blogspot.com ku-install App ya chombohurumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru­­_media


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.