WANANCHI ACHENI MARA MOJA UVAMIZI WA ARDHI-WAZIRI WA ARDHI
WAZIRI wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh.Jerry William Slaa, amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kuvamia maeneo na kumilikishana kiholela badala yake wafuate sheria na taratibu za kumiliki ardhi ii kuepuka migogoro.
Mhe. Slaa ameyasema hayo tarehe 22.09.2023 wakati aipokuwa akzungumza na watumshi wa sekta ya ardhi wa Mkoa wa Morogoro, katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaj wa maagzo ya Baraza la Mawaziri ya kuhakikisha Wizara ya Ardhi inatatua migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi katka maeneo mbalimbali nchin.
“Ni lazima wananch waache mara moja tabia ya kuvamia maeneo. Sheria za ardhi ziko wazi juu ya njia ya kumiliki ardhi. Kama ardhi ni ya kijiji wapeleke kwenye Ofisi ya kijij maombi yao ya kumiliki ardhi na kwa ardhi za mijini, hati ya umiliki inatolewa na Kamishna hivyo mwananchi ye yote anayetaka kumilik ardhi ni lazima afuate sheria za umiliki ili awe salama” alieleza Mheshimiwa Slaa.
Aidha, Mhe. Slaa pia amewataka wananchi waendeleze maeneo wanayoyamiliki huku akiiagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linawasaidia wananchi ambao maeneo yao yamevamwa na kusitiza kwamba dhamana ya kuinda ardhi ya mwananchi haiko mkononi mwa Wizara ya Ardhi bali iko mikononi mwa Jeshi la Polisi hivyo mwananchi ye yote ambaye ardhi yake imevamiwa afike Polis kwa ajili ya kupata msaada.
Kuhusu suala la utatuzi wa migogoro ya ardh, Mheshimiwa Slaa amewataka watumishi wa sekta ya ardhi kuhakikisha migogoro yote inatatulwa ndani ya sku 100 na wanapoitatua wahakikshe wanaweka kwenye maandishi maamuzi waliyoyafikia il kuwa kama ushahidi endapo mbeeni shida yaweza jitokea.
“Fanyeni kliniki za ardhi kwenye maeneo yenu ili mwafikishie wananchi huduma kwa ukarbu zadi. Huduma yenu kwa wateja we nzuri wanapokuja katka ofisi zenu kutaka huduma pia jitahidini kupunguza malalamko ya wananchi kwa kutoa huduma kwa weledi. Mkitenda haki mtapunguza malalamiko madogomadogo yanayoweza kujitokeza” aliagiza Slaa
Naye Kamishna Msaidizi waArdhi Mkoa wa Morogoro, ndugu Frank Minzkunte ametaja usimamizi mdogo wa masuala ya ardhi na uelewa mdogo wa wananch kuhusu urasimshaji wa ardhi, hasa kwenye uchangiaji wa gharama za urasmishaji kuwa ndio vichochezi vikubwa vya migogoro mingi ya ardhi ndani ya Mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo ameiomba Wizara ya Ardh kuongeza bajeti ya ardhi ya Mkoa ili kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa shughui mbalimbali za ardhi ikiwemo upangaji wa mashamba kwa ajili ya kilimo na kutatua migogoro ya ardhi kama vile migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika Wilaya za Kilosa na Mvomero.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment