MKOA WA MOROGORO WAADHIMISHA SIKU YA WAZEE DUNIANI, DC NSEMWA ATOA NENO LA MATUMAINI KWA WAZEE
MKOA wa Morogoro kwa kushirikiana na Halmashauri zake, umeadhimisha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani kwa kukutanisha Wazee kutoka Wilaya zote.
Maadhimisho hayo yamefanyika Oktoba 01/2023 kwenye Ukumbi wa SUA Nanenane Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro .
Akitoa Hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, amewaahidi wazee kuwa Mkoa wa Morogoro utaendelea kutoa vitambulisho vya matibabu kwa ajili ya wazee na kuagiza Idara za Afya katika Halmashauri za Mkoa kuhakikisha zinaimarisha upatikanaji wa dawa katika magonjwa yanayowasumbua wazee.
DC Nsemwa, amesema yale yote ambayo wanawaahidi wazee kutokana na risala yao, yatafanyiwa kazi, ikiwemo kuzielekeza na kuzisimamia Halamshaui ziwawezeshe Wazee ili kujikwamua kiuchumi.
Pia, amezitaka Halmashauri kuhakikisha Vitambulisho vya Msamaha wa Matibabu kwa wazee linakuwa endelevu ili kuwezakuwasaidia Wazee katika matibabu.
Aidha amesema Mkoa wa Morogoro unawategemea wazee ili iweze kupiga hatua kimaendeleo, hivyo kama Serikali ya Mkoa kero na changamoto zao watazifanyia kazi kwa ajili ya ustawi wa Wazee..
Aidha, DC Nsemwa , amewataka wazee kufanya mazoezi ya kutembea kwa kuzunguka maeneo ya nyumba zao au kufanya matembezi mafupi ili kuulinda mwili na kuepukana na magonjwa ya uzeeni.
,"Ni muhimu wazee wakafanya mazoezi ili kulinda afya zao, kwa sababu mazoezi ni tiba tosha ya kuzuia magonjwa pia niwakumbushe wazee kula vyakula vya asili zikiwemo mbogamboga na matunda ya asili kwani vyakula hivyo vina virutubisho vya kutosha" Amesisitiza DC Nsemwa.
"Wazee wanahitaji kuelimishwa kuna lawama tunawalaumu wazee kumbe sisi hatuajawelimisha Mabaraza haya ya wazee yanahitaji sana elimu ya Ukatili na elimu nyengine , Maafisa Ustawi mnapokaa vikao vyenu vya maamuzi juu ya mambo yanayowahusu wazee washirikisheni ili mjue vipaumbele vyao ,mwisho niombe wazee wetu mkalipe uzito suala la utunzaji wa mazingira katika maeneo yenu mnayoishi " Amesema DC Nsemwa.
Kwa upande wa Afisa Ustawi Mkoa wa Morogoro ,Jesca Kagunila, amewashukuru viongozi wa baraza la wazee Mkoa wa Morogoro kwa kukubali kufanya maadhimisho ya siku ya wazee duniani, katika Halmsahuri ya Manispaa ya Morogoro ili kuleta chachu kwa wazee wengine kutambua kuwa wazee wanatambulika katika Mkoa wa Morogoro.
Katibu wa Baraza la Wazee Manispaa ya Morogoro , Dr. Basil Anga, kwa niaba ya Wazee ,ametoa salamu zake kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wazee katika suala la Afya.
Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Kata ya Kihonda Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (A/Insp), Edson Kitanda, amewataka wataalam kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya imani potofu juu ya wazee, ikiwemo mzee kuhusishwa na ushirikina pale anapokuwa na macho mekundu.
"Bila wazee hata sisi tusingekuwa hapa, wazee hawa wamepigaia uhuru na amani ya nchi yetu, ni kosa la jinai kumuita Mzee mchawi, kama kuna watu wanafanya hivyo njooni vituoni au mtupigie simu tutawashughulikia " Amesema Insp. Kitanda.
Tweet@chombo huru media,Youtube@chombo huru media, Facebook@chombo huru media, Instagram @chombohuru_media
Post a Comment