Header Ads

MORO DC MBIONI KUZINDUA VITUO 6 VYA AFYA .

 






HALMASHAURI ya Wilaya ya Morogoro ipo mbioni kuzindua jumla ya vituo 6 VYA afya .

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 29/2021 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Rehema Bwasi, katika Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Bwasi, amesema kuwa mpaka kufikia Februari 25/2021, vituo hivyo vitakuwa vimezinduliwa tayari kwa ajili ya kutoa huduma za afya. 

" Mpaka Sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha vituo hivi, kutokana na Barua ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro wa lini tutavindua, tumepanga tarehe 25/2/2021 ndio uzinduzi rasmi , niwaombe wakazi wa Kata hizo 6 wajiandae kupokea miradi hiyo" Amesema Bwasi.

Kuhusu Hospitali ya Halmashauri, amesema nayo ujenzi umefikia pazuri na wanatarajia hadi kufikia Februari 15/2021, Hospitali hiyo itakuwa ishazinduliwa na tarehe 16/2/2021 huduma za afya zitaanza kutolewa rasmi.

"Vituo vya afya vipo 6, ambavyo ni Kisaki, Mkuyuni, Kisemu, Mikese, Kinonko na Dutumi, kwahiyo matarajio yetu mara baada ya vituo hivi kufanya kazi kutaondoa changamoto ya Wananchi wa Kata hizo kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya" Ameongeza Bwasi.


Naye, Mmoja wa Wananchi katika Kata hizo, Fatma Zuwewe, amempongeza Mkurugenzi huyo , kwani huduma hizo zimekuwa ni kilio Cha muda mrefu kwa wakazi hao.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.