Header Ads

DIWANI MWEMBESONGO AIPONGEZA KAMPUNI YA GUDAL KUSAIDIA UFUKUAJI WA MFEREJI WA ANTI MALARIA.














DIWANI wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, ameipongeza Kampuni ya Gudal,  kufuatia Kampuni hiyo kusaidia Kijiko Cha Burudoza kufukua mfereji wa Anti Malaria uliojaa takataka na mchanga. 

Pongezi hiyo ameitoa leo Januari 20/2021 wakati wa kutembelea eneo hilo. 

Akizungumza Mara baada ya kupokea msaada huo, Mhe. Kalungwana, amesema Mfereji huo ulikuwa ni ni changamoto kubwa kwa wakazi wa Mwembesongo hususani Mtaa wa Gohalema, ambapo wakati wa Mvua umekuwa ukisababisha Mafuriko kutokana na kujaa kwa takataka na mchanga . 


Mhe. Kalungwana, amesema kufukuriwa kwa mfereji huo, kutasabisha Hali ya utulivu kwa wakazi wa Mwembesongo wakati wa Mvua kunyesha. 


" Tunamshukuru Sana Mkurugenzi wa Gudal, Ndugu yangu Hassan Mussa, ametusaidia Sana ametoa kijiko kitakachofukua taka na upanuzi wa mto, naamini baada ya mto huu kufukuriwa Mafuriko Sasa Basi " Amesema Mhe. Kalungwana.

 Aidha, amemshukuru Mkurugenzi Manispaa Morogoro Sheilla Lukuba kwa jitihada za kutafuta wadau wa maendeleo huku akiwaomba wadau wengine wajitokeze kwa ajili ya kusaidia huduma nyengine za Maendeleo.

 Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Manispaa Morogoro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kihonda Maghorofani, Mhe. Hamis Ndwata, amempongeza mdau , huku akisema Sasa muarubaini wa tatizo hilo linakwenda kupatiwa ufumbuzi. 

Pia amewaomba wadau wengine kuendelea kuungana na Manispaa Morogoro kwa ajili ya kusaidia huduma nyengine za Kijamii katika maeneo mbalimbali. 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gohalema,  Orise Rashidi,  amemshukuru Mkurugenzi Manispaa Morogoro Sheilla Lukuba kwani amekuwa mstari wa mbele katika kutatua haraka matatizo ya Wananchi.


 " Mkurugenzi wetu msikivu Sana, tatizo hilo la muda mrefu lakini Mara baada ya kufikishiwa ametafuta mdau kwa kushirikiana na Diwani wetu Mhe. Kalungwana Sasa tunakwenda kuandika historia nyengine, tunaamini Mafuriko yanakwisha, hapa tulikuwa tunalala kwa mashaka na kuomba mvua isinyeshe, lakini kwa kasi ya Serikali ya Sasa ya awamu ya tano Chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, inafanya kazi na sikivu niwaombe Wananchi Mara baada ya mfereji  huu kufukuriwa tusitupe taka hovyo, tutunze vyanzo vyetu kwa afya zetu" Amesema Olise. 


 Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gudal, Hamisi Mussa, amesema wao wameamua kujitolea kusaidia kufukua mfereji huo Mara baada ya kuguswa na tatizo hilo. " Tumejitoa kusaidia Jamii, hili ni janga , hivyo kuishi katika mazingira haya tunahatarisha afya za Watu, niseme tutaendelea kushiriki katika kusaidia Jamii" Amesema Mussa. 

Licha ya Ufukuaji wa mfereji huo, ameahidi kushirikiana na Manispaa kuboresha kivuko kilichopo nyuma ya Ujenzi wa Sheli yao ili kurahisisha huduma usafiri kutokana na Kivuko hicho kuwa sio rafiki kwa matumizi .

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.