Header Ads

MBUNGE ABOOD AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WAFANYABIASHARA MANISPAA YA MOROGORO

      

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (katikati) akikagua eneo la wafanyabiashara wa mboga na vitoweo Soko Kuu la Kisasa Manispaa ya Morogoro, (kushoto) Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (kulia) akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kisasa Manispaa ya Morogoro.


Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba (katikati)  akisikiliza kero za Wafanyabiashara wa Soko Kuu.


MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood,   ameahidi kushirikiana kwa karibu na jumumuiya za wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali  wa Manispaa ya Morogoro katika  kutatua kero zinazowakabili.

Amesema hayo, wakati wa ziara ya kukagua na kusikiliza kero za Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kisasa Manispaa Morogoro leo Januari 04/2021.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema  lengo la ziara hiyo ya  kukutana na  wafanyabiashara ni kwa ajili ya  kujadiliana kwa pamoja juu ya changamoto na fursa za kibiashara zilizopo katika Soko hilo pamoja na Manispaa kwa ujumla.

Mhe. Abood, amesema kuwa serikali bado inautazama Mkoa wa Morogoro  kama miongoni mwa mikoa muhimu katika kukuza uchumi wa mkoa na  taifa kwa ujumla kwa kuzingatia fursa ulizonazo katika rasilimali watu yenye tabia ya kujituma katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, hivyo Manispaa ya Morogoro ina kila sababu ya kujivunia kuwa na sifa hizo katika kuelekea kuwa Jiji.

Aidha Mh. Abood,  amewahakikishia wafanyabiashara  kuwa hoja zao zote walizoziwasilisha katika kujadili fursa na changamoto zitafanyiwa kazi kwa kuzingatia uwezo na mamlaka za maamuzi.

Alifafanua kuwa baadhi ya hoja na changamoto zilizowasilishwa zinaweza kushughulikiwa katika ngazi Manispaa na zingine hususani zinazohusu ngazi ya kitawala na Kijimbo atazishgughulikia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

" Wafanyabiashara wamehamia Sokoni hapa , Soko ni zuri na wengi wameitikia, japo kuna changamoto tumezipata kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro tumezipokea na kwenda kuzijadilia na kuona jinsi  ya kuzitatua ili kuendelea kuwasaidia wananchi kuendelea kufanya biashara" Amesema Mhe. Abood.

Katika hatua nyengine, amesema changamoto zipo kwakuwa Soko ni jipya hivyo watajitahidi kuhakikisha kwamba changamoto zote zinafanyiwa kazi na kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.


Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, amewataka wafanyabisaha kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito kwani kila maendeleo yana changamoto yake.

Kuhusu changamoto ya usafiri wa wafanyabiashara katika Soko hilo, amesema wataruhusu bodaboda 47 tu ambazo zitaruhusiwa kuingia na kufanya maegesho katika Soko hilo ili kuweza kutoa huduma za usafiri kwa Wafanyabiashara.

"Hawa bodaboda 47, ndio watakaokuwa wakiegesha vyombo vyao kwa ajili ya kutumika na wafanyabiashara kwa ajili ya kuelta mizigo yao  wakiwa na sare maalumu za hapa ili waweze kutambulika , lakini kwa upande wa bodaboda watakao kuwa wanapakia abiria watawashusha hapa lakini nje ya soko kwani watakao ingia sokoni ndani ya mipaka ya maegesho watalazimika kutoa shilingi 500 ya ushuru na wale wenye maegesho ya kudumu watalipa shilingi 1000/= kila siku, niwaombe wafanyabiashara huu sio wakati wa malumbano , tufanye kazi , Serikali imetuletea mradi mkubwa wenye gharama lengo kutusaidia sisi na kuborehs maisha ya wananchi wetu" Amesema Lukuba.

Lukuba, amewataka wafanyabiashara  ambao wanafanya biashara zao kando kando ya barabara na maeneo ambayo walitakiwa waondoke wapendekeze eneo la kufanya biashara lakini lisiwe jirani na Soko Kuu ili waone jinsi  ya kuwasaidia .

Pia, ametoa rai kwa wale wenye vizimba wanaopangisha waache tabia hiyo mara moja, laikini na wale wasiofika katika vizimba vyao wafike mwisho tarehe 05/1/2022 kama hawataingia watatafuta watu wengine.



 


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.