MKURUGENZI MANISPAA MOROGORO AWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI
MKURUGENZI Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka Wafanyabiashara Manispaa ya Morogoro kulipa kodi kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya Manispaa na Wananchi kwa ujumla.
Lukuba, amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanawatumia wafanyabiashara wadogo (wamachinga) kuwauzia bidhaa zao ingali wao wanafunga maduka yao kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
"Hawa ambao wanawatumia Machinga kukwepa kodi nitakula nao sahani moja, tutahakikisha kila mfanyabiashara katika Manispaa hii analipa kodi, hatuwezi kuishi kienyeji namna hii harafu tuwe tunawaangalia, Mhe. Rais anapambana na miradi mikubwa ni kwa sababu ya kodi za wananchi, tupo kazini na tuatendelea kuwafauatilia wanaojificha kupitia mgongo wa Wamachinga , tukiwabaini hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Amesema Lukuba
Aidha, amesema , Nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi hata miradi mikubwa ya Kimkakati inayotekelezwa katika Manispaa hiyo imetokana na kodi za Wananchi .
"Niwaase wafanyabiashara, hakuna njia za mkato, Serikali inahitaji kodi ili iendelee na miradi mingine mipya , niwaase tulipe kodi kwa ustawi wa maendeleo ya nchi kwani miradi mingi ya maendeleo inategemea kodi za wananchi,hivyo niwatake wamachinga kutokukubali kutumiwa na wafanyabiashara wakubwa ili wakwepe kodi" Ameongeza Lukuba .
Amesema elimu pia inaitajika kwa wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji kodi kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Post a Comment