DC MSULWA AWATAKA MADIWANI MANISPAA MOROGORO KUFANYA KAZI KWA MAADILI KULETA MAENDELEO.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa umakini Mkutano wa Baraza la Madiwani.
WAHESHIMIWA Madiwani Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutambua kuwa ili kuwa na utawala bora wanao wajibu wa kushugulika na changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuhakikisha vikao vya kisheria vinafanyika inavyostahiki kwani vikao hivyo ni njia mojawapo ya kushughulika na kero za wananchi lakini pia kujiletea maendeleo katika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, wakati akitoa salam zake katika baraza la madiwani leo Januari 28/2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Stendi ya Mabasi Msamvu.
Akizungumza na Waandishi wa habari, DC Msulwa, amewataka Madiwani kuhakikisha wanasoma kanuni za Halmashauri na taarifa mbalimbali zinazotoka kwa wataalam lakini pia kujenga ushirikiano katika kutatua kero mbalimbali pamoja na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na Serikali Kuu ili halmashauri iweze kwenda vizuri.
DC Msulwa, amesema anatambua kazi kubwa iliyofanyika katika ukusanyaji wa mapato kwani kipindi cha mwaka 2020 /2021ambapo hali ya makusanyo ya mapato ilikuwa billion 8 wananchotakiwa ni kuongeza kasi katika kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuendelea kusimamia, kukusanya na kuvifikia vyanzo vyote vya mapato ambavyo havijafikiwa .
Aidha, lakini pia amewataka madiwani kushirikiana na Halmashauri kuwa na mpango mkakati wa kuandaa master plan ya mji kwani kwani shughuli mbalimbali zitaongeza kupitia ujenzi wa reli ya mwendo kasi unaoendelea ambapo inategemewa kuwa na ongezeko la watu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
"Ndugu zangu dhamana muliyopewa ni kubwa sana hamjatumwa huko halimashauri kwenda kujinufaisha nyinyi na familia zenu nendeni mkatekelezeyale mlioahidi ili kurudisha heshima muliyopewa na wananchi, tunatarajia kuwa Jiji , hatuwezi kuwa Jiji kama bado tuna malumbano, lazima tuwe kitu kimoja tufanye kazi kama timu na kuongeza vyanzo vya mapato ili tuboreshe miundombinu yetu bila kutegemea ruzuku kutoka Serikali Kuu " Amesema DC Msulwa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Sabasaba, Mhe. Mohamed Lukwale, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho cha Baraza la Madiwani, amewataka madiwani wenzake pamoja na Watumishi wa Halmashauri kumpa ushirikiano wa kutosha Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro katika kusimamia makusanyo na matumizi ya fedha kutoka Serikali Kuu na Halmashauri ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mhe. Lukwale, amesema kuwa dhamana na heshima waliyopewa madiwani na Wananchi ni kubwa mno na isiyoelezeka na jambo ambao anaweza kuahidi katika Baraza hilo ni ushirikiano wa kutosha katika kuleta maendeleo.
""Natambua uchaguzi huu ulioisha tulipitia mambo mengi sana ,lakini sasa uchaguzi umekwisha ni mwendo wa kuchapa kazi sasa twende kuchapa kazi ili turudishe ile heshima tuliyopewa na wananchi wetu kwa kutuchagua " Amesema Mhe. Lukwale.
Mwisho, Mhe. Lukwale, amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa , Sheilla Lukuba, pamoja na watendaji wote kuhakikisha wanashirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha wanatatua na kumaliza kero zote zinazowakabili wananchi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema kama viongozi wanao wajibu wa kuweka mazingira bora ya kujifunza kwa ajili ya kizazi chetu katika sekta ya elimu msingi, sekondari na vyuo kwa kuhakikisha kunakuwa na huduma bora na mazingira mazuri ya kujifunzia lakini pia kuhimizana katika kuwekeza katika kubuni vyanzo vipya vya mapato sambamba na kuchochea maendeleo.
Lukuba, amewasihi Madiwani hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kuifanya Manispaa hiyo iwe na uwezo wa kujiendesha na kuhudumia wananchi wake.
Kuhusu uhaba wa vyumba vya madarasa kwa kidato cha kwanza, amesema kuwa Waheshimiwa madiwani ambao ndiyo wenyeviti wa kamati za maendeleo katika kata wahakikishe wanashirikiana na viongozi wote katika kata zao ili kuhamasisha maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa ili vijana waliochaguliwa kidato cha kwanza waweze kujiunga na masomo kama ilivyokusudiwa.
Pia,ametaka kila kata iwe na mpango mkakati wa kudumu kwa kuweka mipango mapema mara tu vijana wanapojiunga darasa la kwanza kwa uongozi wa kata kuanza kufikiria mahitaji ya kielimu mapema na isiwe kama zimamoto.
Naye, Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Maulid Chambilila, amewataka madiwani hao kuwa waadilifu na kukumbuka wana deni la kutatua kero za wananchi .
Chambilila, amesema kuwa wananchi hao wamewapa dhamana kubwa ya kuwatumikia hivyo wanapaswa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.
" Wananchi wamewaamini sana kwa kuwapa dhamana ya kuwaongoza, wekeni maslahi ya wananchi mbele, kama mna changamoto zenu zipo sehemu za utatuzi wa hizo changamoto na msianze malumbano ambayo hayana tija, tafuteni mbinu mbadla aambazo zitaweza kuisogeza Manispaa mbele na kututoa hapa tulipo, shirikianeni na Wataalamu ili wale waliowapa dhamana waone matunda yenu, mkianza malumbano hata wale waliowachagua hamtawatendea haki na miaka mitano ijayo tutakuwa katika hali ngumu sana , moja ya sifa ya kuongozi wa umma ni kuweka maslai ya wananchi wake mbele kwanza kabla ya mashali yake, kwani kiongozi yuko kwa ajili ya kuhudumia watu na sio yeye binafsi" Amesema Chambilila.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika mkutano huo wa kawaida wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro, ni pamoja na Mkuu wa Wialaya ya Morogoro, Viongozi wa Chama Wilaya Morogoro Mjini , Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro , Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wanachi.
Post a Comment