Header Ads

MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO WATAKIWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO.

 

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Wilaya ya Morogoro Mjini, Maulidi Chambilila,  akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa  Mikutano wa Stendiya Mabasi Msamvu.

MADIWANI katika  Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro iliyopo katika maeneo yao badala ya kuwa chanzo cha migogoro hiyo.

Wito huo umetolewa leo Januari 28/2021 na Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Wilaya ya Morogoro Mjini, Maulidi Chambilila,  wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa  Mikutano wa Stendi ya Mabasi Msamvu.

Akizungumza na Waandishi, Chambilila, amewataka Waheshimiwa  madiwani watumie hekima,busara na vipaji wwalivyojaaliwa na mungu kuhakikisha migogoro inamalizika kwa Amani na kuwaletea Wananchi maendeleo.

Chambilila, amesema kuwa  kazi iliyopo kwa sasa ni kuleta maendeleo kwa wananchi na changamoto zilizopo Manispaa ya Morogoro  zitumike kama fursa za kusogeza mbele Manispaa  kimaendeleo na sio sehemu ya kulalamika na kuona kwamba haiwezekani kuvuka katika jambo hilo.

Aidha, amesema kuwa  wananchi wana matumaini makubwa ndiyo maana waliwaamini na kuwachagua,hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuchapa kazi kwa maendeleo ya jamii.

Tuchape kazi na kila mmoja aone ana wajibu wa kuhakikisha anakwenda kuwatumikia wananchi,sote tusimame kama timu moja kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Manispaa yetu ya Morogoro”Amesema Chambilila.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.