MBUNGE ABOOD AKABIDHI VIFAA VYA SHULE VYENYE THAMANI YA MILIONI 13 KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe Abdulaziz Abood, amekabidhi vifaa vya Shule vyenye thamani ya shilingi Milioni 13 kwa wazazi wa wanafunzi 62 waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza Shule mbalimbali wanaoishi ndani ya Jimbo la Morogoro Mjini.
Zoezi hilo limefanyika Januari 05/2021 katika Ofisi yake wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Jimbo lake kama ilivyo kawaida yake na ratiba aliyojiwekea.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Wazazi wa Watoto hao,Mhe. Abood, amewasihi wazazi wahakikishe watoto hao wanaenda Shule na kusoma vizuri kwani Serikali inahitaji watoto wote wasome na ndiyo maana imefuta ada kwa wanafunzi Shule za Msingi na Sekondari kidato Cha kwanza mpaka Cha nne.
''"Tumeona tuanze na hawa wachache 62 lakini huu ni msaada amabao tumeotoa kwa wale wenye uhitaji mkubwa zaidi tumezingatia shida za hawa wananchi na tulaiahidi leo tumeona tutekeleze , kikubwa niwaase wazazi wasimamieni watoto wenu katika masomo, mwalimu awe mtu wa kati, fuatilieni taaluma za watoto wenu, mwalimu atamlea mtoto shuleni na nyumbani wewe una wajibu wa kutimiza majukumu yako, wasome na watimize malengo, Serikali ya Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli, inahitaji watoto wote wasome na ndiyo maana imefuta ada kwa wanafunzi Shule za Msingi na Sekondari kidato Cha kwanza mpaka Cha nne" Amesema Mhe. Abood.
Miongoni mwa vifaa alivyokabidhi kwa wazazi wa wanafunzi hao ni pamoja na Madaftari, Viatu, Mabegi, Uniform, Kalamu, Penseli na fedha Taslimu.
Katika hatua nyengine, Mhe. Abood, amekabidhi baiskeli kwa baadhi ya Vijana wenye Ulemavu ili ziwasaidie katika Shughuli mbalimbali zikiwemo za Shule.
Post a Comment