Header Ads

DIWANI KANGA ACHANJA MBUGA, WANANCHI WAJAWA NA MATUMAINI









 Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akiendelea na ziara ngazi ya Mitaa ya Mikutano ya wazi ya hadhara katika kusikiliza na kutatua keto za Wananchi wa Kata ya Kilakala, leo Janiari 16/2021 akiwa katika Mitaa ya Kigurunyembe,Kigurunyembe, kigurunyembe mizambaraun, Mahedu, Migomban, Kola, Ng'atigwa ikiwa na lengo la  kuwashukuru Wananchi kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwa Diwani lakini kuwashirikisha Wananchi katika kuchangia miradi ya maendeleo na kutoa maoni jinsi ya kuendesha Kata hiyo, lakini kubwa kukusanya maoni, changamoto kabla ya kwenda katika Baraza la Madiwani Manispaa Morogoro kuwasilisha kero hizo. 

Mhe. Kanga, amejiwekea ratiba hiyo ili kupunguza kero na Msongamano wa Wananchi kufuata ufumbuzi ngazi ya Manispaa Morogoro. 

Aidha, amesema maendeleo ya Kilakala yataletwa na Wanakilaka wenyewe. 

Amewataka Wananchi kujenga desturi ya kuhudhuria katika Vikao ili kuamua hatima ya Kata yao na maendeleo kwa ujumla..

1 comment:

  1. Sawa shukurani kutujulisha! Alipokea maoni gani toka kwa Wananchi!!

    ReplyDelete

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.