Header Ads

MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA



 

Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha kuwasilisha taarifa za Kata zao.

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwale , akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, katika kikao cha kuwasilisha taarifa za Kata.

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Mohamed Lukwale ,akifungua kikao cha uwasilishaji wa taarifa za Kata kwa Madiwani.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,akiwa katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa za Kata .

Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Mhe. Emmy Kiula, akiwasilisha taarifa za Kata yake.

Diwani wa Kata ya Mwembesongo,  Mhe. Ally Kalungwana , akiwasilisha taarifa za Kata yake.

MADIWANI wa Manispaa ya Morogoro,  wamefanya  mkutano wa kuwasilisha taarifa za kata za ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani litakalofanyika tarehe 28/1/2021.

Mkutano huo wa kuwasilisha taarifa , umefanyika leo Januari 26/1/2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimo,

Mkutano huo umehudhuriwa na madiwani wa kata zote 29 pamoja na Watendaji wa Kata ,  Wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Madiwani hao waliweza kuwasilisha  taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio  na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji,  utekelezaji  wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi na afya.

Hata hivyo baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni  pamoja uhaba wa maji , miundombinu ya barabara, ukosefu wa vyoo katika baadhi ya shule n.k.

Mwisho , taarifa zote ambazo ziliwasilishwa katika Kikao hicho ambacho kiliendeshwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro ambaye ni Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa, Mhe. Mohamed Lukwale, pamoja na  Katibu wa kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, zilipokelewa.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.