WAITARA ARIDHISHWA NA USAFI MANISPAA YA MOROGORO, ATAKA KASI IONGEZWE KATIKA UPATIKANAJI WA DAMPO LA KISASA
Afisa Dampo, Alex Roman (wapili kutoka kulia) akisikiliza kwa makini maelekezo ya Mhe. Waiata ya kuboresha dampo.(wapili kushoto), Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga. (katikati), Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba.
Mhe. Diwani wa Kata ya Mafisa, Mhe. Joelly Kisome (kushoto), akizungumza na Mhe. Waitara mara baada ya kuwasili Dampo la taka Manispaa ya Morogoro.
Afisa Mazingira Mkoa wa Morogoro, Venance Soza Segere, akisoma taarifa ya Mazingira Mkoa wa Morogoro.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa mipango mizuri na usimamizi mzuri wa usafi huku akitaka nguvu iongezwe katika ufuatiliaji wa Dampo la Kisasa.
Kauli hiyo, ameitoa leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Dampo la taka Manispaa ya Morogoro lililopo Kata ya Mafisa.
''Nimefurahishwa sana na hali ya hatua za kuanza kutekeleza ujenzi wa Dampo la Kisasa, mmeniambia tayari andiko lipo na mshaliwasilisha kazi yangu mimi ni kusukuma ili hizo fedha zitoke, lakini niwaombe Dampo la kisasa lizingatie miundombinu yote, lisiwe kama hili la kienyeji hapa tushakosea kikubwa kuhakikihsa wakati tunajiandaa na ujenzi wa Dampo Jipya , hili tulilo nalo tuliwekee mazingira rafiki taka zisibaki nje, hapa kuna taka zipo ambazo zinazalisha sumu, haya maji yakitiririka yanawafikia wananchi na ni hatari kwa afya,
Aidha, amesema sio jambo baya Manispaa ikatoka ziara kwa ajili ya mafunzo ya kuona wenzao walivyojipanga katika ujenzi wa Madapo lakini hata katika usafishaji wa Mji .
Mhe. Mwita, amesema kutohudumia dampo hilo ipasavyo kunapelekea uchafuzi wa Mazingira harufu mbaya, na maji yenye sumu kali na kuhatarisha afya ya wakazi wa maeneo jirani viumbe hai na mzingira kwa ujumla.
“Nawapongeza sana kwa hatua hii ya kuanza kubuni mchakato wa utekelezaji wa mradi wa Dampo jipya, lakini kwa hatua nzuri za usimamizi mzuri wa usafi, kama mlivyosema mataka kwenda jiji, hatuwezi kuwa Jiji wakati bado kuna taka zinazagaa mitaani, jipangeni vizuri, mmesema mshawasilisha taarifa na andiko la mradi wenu, tutasukuma kuona hizo fedha zinatoka ilia ujenzi uanze, kisha ujenzi huo uzingatie miundombinu mizuri ya Dampo, lakini kikubwa zaidi endeleeni kutoa elinmu kwa wananchio wenu jinsi ya kutengeanisha taka nyumbani ili waone taka ni dili na sio uchafu mara baada ya kuanzisha kiwanda chenu cha uchakataji wa takataka" Amesema Mhe. Waitara.
Katika ziara hiyo ameitaka Halmashauri kuwa na mikakati mizuri ya kusimamia usafi ikiwamo kuwa na mbinu bora za kufanya kila mmoja kuona jukumu la usafi ni lake na kuwa na sheria ambazo zitatekelezwa kwa asilimia mioa moja katika usafi ikiwamo na tozo za usafi na faini kwa wale waharibifu wa mazingira.
Post a Comment