Header Ads

DIWANI KANGA AHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO, AWATAKA WANANCHI KILAKALA KUMPA USHIRIKIANO.


















DIWANI wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amehitimisha ziara yake katika Mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero za Wananchi katika Mitaa Bwinila, Nugutu , Charumbi, Mbogo,  Kilakala na Bon'gola kwa kishindo huku akiwataka Wananchi kumpa ushirikiano. Mkutano wake amehitimisha leo Januari 17/2021 katika Eneo la Kiwanja Cha Mpira  Mtaa wa Nugutu.

 Kanga, amesema baada ya ziara hiyo ataunda Kamati mbalimbali zitakazoweza kusaidia kusukuma gurudumu la Maendeleo ya Kata ya Kilakala. 

" Nimehitimisha ziara yangu ya Mikutano ya wazi, yapo maelekezo nimeyatoa kwa Watendaji wa Mitaa , changamoto nimezipokea lakini siwezi kuzitatua Kama mzigo huu mkiniachia peke yangu, tushikane mikono na tuwe kitu kimoja ili haya ambayo tumeyazungumza tuyafanyie kazi" Amesema Mhe. Kanga. 

Aidha, amewataja Watendaji wa Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuanza nao kufanya Mikutano ya hadhara ili kupunguza msongamano wa Wananchi katika Ofisi za Kata na Manispaa.

 Amesema kwa Sasa ataanzisha mtandao maalumu Wenye kujumuisha wataalamu mbalimbali katika Mitaa ikiwemo Wastaafu na wasio staagu ili kusaidia kutengeneza mipango Bora ya Maendeleo ya Kilakala. 

Mwisho , amewashukuru Wananchi wa Mitaa yote Kata ya Kilakala kwa kujitokeza kwa wingi katika Mikutano huku akiiahidi kutowatupa na kuwaapa ushirikiano wa kutosha ili kutekeleza vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020-2025.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.