Diwani Kanga, afufua matumaini ya ukarabati Soko Kilakala.
Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Mahedu.
DIWANI wa Kata ya Kilakala ,
Mhe. Marco Kanga, amefufua matumaini ya
ukarabati wa Soko la Kilakala Mara baada
ya kupokea changamoto zinazoikabili Soko hilo kutoka kwa Viongozi.
Kauli hiyo, ameitoa Januari
05/2021 wakati wa Mkutano wa hadhara wa wazi katika Mtaa wa Mahedu wa
kusikiliza na kutatua kero za Wananchi ambapo alialikwa kwa ajili ya kusikiliza
Wananchi.
Akizungumza kuhusu Soko hilo,
amesema kuwa Manispaa imetenga milioni 20
, kwa ajili ya ukarabati , hivyo wananchi wawe na matumaini makubwa ya kuanza
kunufaika na mradi huo.
" Mradi umechelewa sana , niwaombe ndugu zangu, Mkurugenzi ameshatutengea milioni 20 na Mbunge wetu Mhe. Abood ametusaidia kiasi cha Shilingi milioni 1,000,000/= kwa ajili ya uboreshaji wa Vyoo, hivyo nitahakikisha nalisimamia hili kuona Soko hili linafanyakazi mapema na kuongeza pato la Wananchi wetu wa Kilakala hususani wale wafanyabiashara pamoja na Kuingizia mapato pia Manispaa ya Morogoro kutokana na ukusanyaji wa ushuru katika Soko hili, ” Amesema Kanga.
Hata hivyo , Kanga, amesema kuwa baada ya kupata fedha hizo amewataka watakao simamia ukarabati wa Soko hilo, wahakikishe wanafuata taratibu na Sheria za kutoa pesa hiyo kwani pesa za Serikali zina utaratibu wake katika matumizi .
Kanga, amesema , kukamilika kwa Soko hilo kutachochea maendeleo ya Kata ya Kilakala na kuwafanya wafanyabiashara kutosafiri umbali wa muda mrefu kufuata huduma mjini, lakini hata wauza matunda wataongeza kasi ya uzalishaji kutokana na Soko hilo.
Pia, amesema ataunda kamati ya kuangalia upya wale wenye fremu Sokoni ili kuona ni namna gani ya kuweza kuyatumia maeneo hayo kwa wale wambao wameyatelekeza maeoeno yao na wasio na sifa za kuwa katika Soko hilo.
Kuhusu suala la usalama, amesema suala hilo ni Mtambuka hivyo sio kwa Mtaa wa Mahedu pekee bali ni Kata nzima jambo ambalo amehaidi kulifanyia kazi ikiwemo ujenzi wa Kituo kidogo cha Polisi kwa kuwa eneo lipo tayari kilichobakia ni bajeti na utekelezaji.
Hata hivyo, amewataka Wataalamu washuke chini
katika vikao vya hadhara ili waweze kujibia kero za wananchi, badala ya kukaa
Ofisi na kuongeza mrundikano wa Wananchi
kufuata hudma katika Ofisi ya Kata.
“Hawa Wataalamu ndio wenye majibu ya hizi kero, lazima washuke chini wasikae Ofisini pekee, hawa wananchi ndio waajiri wetu lazima tuhakikishe kwamba kero zao tunazifanyia kazi, tunataka wananchi hawa wajue kila kitu kinachoendelea katika Mitaa na Kata yao kwani wamekuwa na imani kubwa na sisi hivyo lazima tufanye kazi kwa Kasi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwatumikia wananchi kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi” Ameongeza Kanga.
Katika hatua nyengine,
amewataka Vijana, Wakina Mama na Watu wenye ulemavu wake katika vikundi ili
waweze kupatiwa mikopo kwani Manispaa imetengea zaidi ya Milioni 700 kwa ajili
ya mikopo.
Aidha, Mhe. Kanga, amewataka Wananchi kuchangia miradi ya maendeleo ikiwemo kuhakikisha Kata hiyo ina kuwa na Ujenzi wa Ofisi za Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kusogeza huduma karibu na Wananchi.
Mwisho, amesema , katika kuhakikisha Kata hiyo
inabadilika, amekusudia kuboresha miundombinu ya barabara, Maji , Soko pamoja
na Huduma za afya katika kipindi chake cha kwanza cha miaka 5 madarakani.
Post a Comment