Header Ads

MEYA KIHANGA AWACHARUKIA WAALIMU WAKUU, AWATAKA WAJITATHIMINI.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga akisalimiana na Viongozi wa Kata ya Mzinga mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Konga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa na maendeleo ya elimu.


Shule mpya ya Msingi Konga Kata ya Mzinga ambayo imejengwa kwa mapato ya ndani.



Vyumba vipya vya madarasa Shule ya Sekondari Kihonda.


Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari, Sumaye .

Ujenzi wa Madarasa 2 ya Shule ya Sekondari Sumaye Kata ya Bigwa.




Ujenzi wa madarasa 4 mapya katika Shule ya Sekondari Lupanga Kata ya Kilakala.







 

MSTAHI Meya wa Manispaa na Diwani wa Kata ya Mazimbu, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Walimu wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, kujitathimini na kuona Kama wanafaa kukaa Manispaa Morogoro.

 Kauli hiyoameitoa leo Januari 19/2021 wakati wa ziara ya kikazi ya Ukaguzi wa vyumba vya Madarasa vilivyojengwa na Manispaa Morogoro kufuatia agizo la Serikali la kutaka Wanafunzi wote kuingia darasani. 

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Kihanga, amesema kumekuwa na matokeo mabovu ambayo hayaridhishi Jambo linalopelekea Manispaa hiyo kushika nafasi za nyuma huku ikiwa mjini.

 Mhe. Kihanga, amesema kuwa, sasa ni wakati wa Waalimu hao kuanza kujitathimini upya kutokana na matokeo hayo. 

" Nimeanza ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Shule na vyumba vya Madarasa, lakini matokeo bado hayaridhishi hususani katika upande wa Sekondari, tunashindwa hadi na wenzetu wa Kijijini, sisi tuna kila kitu lakini wapi tuna kwama? Hizi nafasi sio zetu, niwaombe Waalimu mjitathimini, Serikali inawekeza katika ujenzi na nyinyi tunataka matokeo mazuri, baada ya ujenzi wa madarasa tunahamia kwenu, Kama umeshindwa kukaa Manispaa ondoka kabisa, tunataka matokeo mazuri tufanane na hadhi yetu ya Manispaa" Amesema Mhe.Kihanga. 

 Amewataka Waalimu wakuu wanapokaa katika vikao vyao wamualike ili wazungumze kwa pamoja na kuona changamoto ambazo zipo na kuzitatua. Suala la Waalimu, amesema kuwa, Mpango uliopo kwa Sasa ni kuongeza Waalimu wa Sayansi ambao ndio changamoto kwa Sasa. Kuhusu Ujenzi wa Shule ya Msingi Konga, amempongeza Sana Mkurugenzi Manispaa Morogoro Sheilla Lukuba, kwa jitihada za kupambania Sekta ya elimu, kwani Sasa amekuwa akitoa fedha nyingi katika kata kwa ajili ya maendeleo mbalimbali ikiwemo suala elimu. 

" Mkurugenzi wetu anajitahida Sana , tumtumie vizuri, anahangaika Sana, sisi hatuhitaji kubweteka, tufanye kazi, haya matokeo yanatuumiza Sana, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wote tunaumia, huu ni muda wa kujipanga Sasa tutoke hapa tulipo twende mbele"Ameongeza Mhe. Kihanga.

 Mwisho , amesema kuwa ziara hizo zitakuwa endelevu, lakini kwanza ameanza katika Shule za Sekondari  baada ya hapo atahamia Shule za Msingi. Miongoni mwa Shule alizoanza nazo ziara ni pamoja na Shule ya Msingi Konga Kata ya Mzinga, Shule ya Sekondari Kihonda Kata ya Mazimbu,  Shule ya Sekondari Sumaye Kata ya Bigwa na Shule ya Sekondari Lupanga Kata ya Kilakala. 

Naye Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, amemshuku, Mstahiki Meya kwa ziara hiyo huku akimuahidi kumpa ushirikiano na kuhakikisha anafuatilia kwa ukaribu Hali ya elimu katika Kata hiyo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.