Header Ads

MANISPAA ILALA YASHEREKEA SIKU YA MAPINDUZI KWA KUFANYA BONANZA LA VIJANA NA UCHANGIAJI WA DAMU .









 
Katika kuyaenzi na kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika chini ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Visiwa hiyo hayati Abeid Aman Karume, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imefanya bonanza la vijana kwa vikundi mbalimbali vya jogging katika Manispaa hiyo kwa ajili ya kusherehekea Mapinduzi hayo, sambamba na uchangiaji Damu kwa hiari.


Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Usikate tamaa vilivyopo vigunguti katika Manispaa hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo ambaye pia ni Diwani wa Vigunguti Omary Kumbilamoto alisema kuwa vijana wamejitokeza kuenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa vitendo kutokana na kupata elimu ya kutosha ya umuhimu wa Mapinduzi hayo.


Aidha aliendelea kusema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala itahakikisha inawasidia kuwainua vijana kiuchumi kutokana na kuwapatia mafunzo maalumu ya ujasiliamari pamoja na kuwapatia mitaji kutokana na soko la ajira kuwa changamoto kubwa kwa vijana hapa chini.


" Elimu ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar vijana wengi wameifahamu ,ndiyo maana vijana wengi wa jogging wamejitokeza kusherehekea miaka hamsini na saba ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar" alisema Kumbilamoto.


Kwa upande wake Mtaalamu  wa maabara kitengo cha Damu Salama kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Ndonya Hussein alisema kuwa katika bonanza hilo wamefanikiwa kukusanya Damu zaidi ya uniti hamsini kutokana na mwitikio mkubwa wa vijana kujitokeza kuchangia Damu kwa hiari.


Alisema kwamba hali ya upungufu wa damu kwasasa inapungua kulingana na mwitikio mzuri wa wananchi katika kuchangia Damu ambayo inatumika kwa watu wenye matatizo mbalimbali Kama vile ajari,seli mundu,na wakina mama wajawazito.


"Tunaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhamasika kuchangia Damu kwa hiari ili kusaidia kuokoa maisha kwa wagonjwa na wenye   uhitaji mkubwa wa   Damu" alisema Ndonya.


Bonanza hilo ni mara ya kwanza kufanyika katika Manispaa hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kukumbuka mchango wa viongozi waliopigania uhuru na kuuondoa utawala wa kisultani katika visiwani Zanzibar.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.