Wananchi wa Kata ya Kilakala wakipata lishe.
Mtendaji wa Kata ya Kilakala, Amina Saidi, akipika uji kwa ajili ya kuwagawia watoto .
MTENDAJI wa Kata ya Kilakala, Amina Saidi, ametaka wadau wa lishe kupambana kutokomeza udumavu ndani ya Manispaa ya Morogoro hususani wakazi wa Kata ya Kilakala ili kuwa na jamii bora isiyo na udumavu .
Kauli hiyo imetolewa Januari 24/2021 katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Kata ya Kilakala iliyofanyika katika eneo la Soko la Kilakala.
Akizungumza jana wakati wa maadhimisho hayo, Amina ,amesema kuwa Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Manispaa ambazo hazina shida ya vyakula, hivyo si sahihi Kata ya Kilakala ikawa na tatizo la udumavu wakati chakula kipo cha kutosha .
" Kwanini Kilakala tuendelee kuwa na uduamavu wakati tunalima matunda ya kutosha ,tuna wanga wa kutosha na mboga za majani za kutosha tuna kila aina ya virutubisho vya mwili tumekuwa na changamoto ndogo ndogo ambazo zilikiukwa toka zamani ila sasa ni wakati mzuri wa kuzifanyia kazi changamoto hizo " alisema
Alisema moja kati ya changamoto kubwa ya baadhi ya wazazi kutozingatia utunzaji mzuri wa watoto wakati wakiwa na ujauzito na baada ya ujauzito kwa kushindwa kulea watoto kwa kipindi cha siku 1000 kama inavyotakiwa kwa mtoto kutunzwa .
Amina, alisema kuwa suala lishe limekuwa na tatizo mtambuka katika Taifa , hivyo ni wajibu kwa wadau wote ndani ya Kata ya Kilakala kupambana na suala la lishe .
Kuwa taifa linapokuwa na watu wengi wenye udumavu ni hatari sana kwa Taifa linakosa watenda kazi wazuri hivyo ni lazima kujipanga kuona suala la lishe linapewa kipaumbele kama njia ya kuondokana kabisa na changamoto ya lishe na udumavu ndani ya Kilakawilaya .
Alisema hali ya lishe inapaswa kuongezwa zaidi ili kuona jamii inatumia vema vyakula vinavyo zalishwa katika wilaya hiyo kama sehemu ya kuongeza lishe bora kwa jamii .
Akizungumza kwa njia ya simu, Diwani wa Kata ya Kilakala,Mhe. Marco Kanga, alisema kuwa sababu kubwa inazosababisha hali hiyo ni kutowekeza muda wa kuwa na watoto kuwalisha ipasavyo ikiwepo kuwapa pombe kwa baadhi ya maeneo, lishe duni kutokana na wananchi kutokuwa na elimu ya ulaji wa chakula cha kutosha na chenye mchanganyiko wa viini lishe.Kanga, alisema kuwa kuwa kutokana na changamoto hiyo, Kata ya Kilakala , inatarajia kuweka mikakati mbalimbali katika kuweza kupambana na hali ya utapiamlo na udumavu kwa watoto wenye chini ya miaka mitano ikiwemo kutoa elimu ya nadharia na vitendo kwa jamii kuhakikisha kwamba ulaji wa kiwango cha juu cha virutubishi unafanyika na kuzingatia unyonyeshaji katika siku 1,000 za mtoto unafuatwa.
Post a Comment