Header Ads

DIWANI KILAKALA AANZA ZIARA YA KUSIKILIZA KERO, WANANCHI WAAHIDI KUMPA USHIRIKIANO.

 

Diwani wa Kata ya Kilakala, Mhe. Marco Kanga, akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.


                                
 

DIWANI wa Kata ya Kilakala , Mhe. Marco Kanga, ameanza ziara za kutembea Mtaa kwa Mtaa kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Ziara hiyo ,ameianza Januari 15/2021 katika Mitaa 3 ikiwamo Mtaa wa Ualimu, Bigwa Sokoni na Bigwa Kisiwani.

Akizungumza na Wananchi wa Mitaa hiyo, Mhe. Kanga, amewataka Waananchi kuhudhuria mikutano inayoitishwa ili kuweza kuchangia maendeleo ya Mitaa yao.

Mhe.Kanga, amesema kuwa, lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha anakusanya maoni kabla ya kuayawasilisha katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro.

Kuhusu, Maji, amesema tayari kuna miradi mikubwa inatekelezwa hivyo ni suala la muda tu na kuwa wavumilivu kwani Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt John Magufuli ni sikivu na inafanya kwa vitendo.

Akizungumzia juu ya barabara, Mhe. Kanga, amesema wapo katika mpango wa kuandaa kamati ndogo ya kupitia barabara zote zilizopo katika Mitaa ili ziiingizwe TARURA.

“Nimeanza ziara yangu ya kwanzqa katika Mitaa hii 3, lakini bado nitaendelea na ziara kuhakikisha naifikia mitaa yote iliyopo katika Kata yangu, huu ni utaratibu ambao nimejiwekea katika Ofisi yangu kwa kushirikiana na Mtendaji wangu wa Kata yakuzunguka mitaa yote kukusanya changamoto, kero na maoni kabla sijafkisha Halmashauri, niwaombe ndugu zangu vikao ni muhimu, Kilakala itajengwa na sisi wenyewe, hakuna mtu wa nje atakayetujengea Kilakala, tushiriki katika maendeleo ili tupige hatua zaidi kwa ustawi wa Kata yetu na Wananchi wenyewe” Amesema Mhe. Kanga.

Suala la Soko, amesema tayari Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ameshaahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuboresha miundombinu iliyobakia ikiwemo suala la vyoo kwa wafanyabiashara wa Soko la Kilakala huku Mhe. Abood akiwa kashachangia shilingi milioni 1 katika uboreshaji huo wa Soko.

Kuhusu hoja ya ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari Lupanga na Kingaru, baada ya kuwasilisha Wananchi wote walikubaliana kwa kauli mbiu moja ya kukusanya michango ambayo itasaidia kupatikana kwa Maabara katika Shule hizo.

“Sula la michango ya ujenzi wa Maabara katika shule zetu hizi, nimewasilisha na wananchi kwa kauli moja wameahidi kuchanga kila kaya shilingi 10,000/= kwa awamu mbili yaani kila mwezi shilingi 5000/= lakini fedha hizo tutaomba ziwe chini ya ukusanyaji wa Ofisi ya Mkurugenzi ili kuwe na uhuru zaidi na uwazi kwa wananchi, kilichobakia hapa ni Mtendaji wangu wa Kata kuandika baarua ya kuomba kibali cha kuchangisha kupitia kwa Mkurugenzi wa Manispaa kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kasha tuanze zoezi hilo mapema ili kutengeneza wanasayansi katika shule zetu” Ameongeza Kanga.

Pia, amesema tayari eneo la wazi katika Mtaa wa Ualimu limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi kidogo ili kuimarisha ulinzi katika Kata ya Kilakala.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Mitaa hiyo, Juma hamisi, amesmshukuru Diwani kwa kuwatembelea wananchi na kujua kero zao huku akiwataka Wananchi wenzake kuendelea kumpatia ushirikiano Mhe. Diwani ili Kata yao isonge mbele katika Maendeleo.

Ziara hiyo itaendelea tena, Januari 16/2021 katika Mitaa ya Kiguru Nyembe, Mizambarauni , Kola , na Ng'atigwa.

 

 

 

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.