WATAFUNAJI WA FEDHA ZA TASAF WAONYWA
Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, (National Steering Committee ) Eng. Rogatus Mativila, akikagua zoezi la uhakiki wa Kaya zilizo katika Mpango wa TASAF . |
Zoezi la uhakiki Kaya zilizo katika Mpango wa TASAF likiendelea. |
WATAFUNAJI watakao bainika kufuja fedha za walio katika mpango wa TASAF kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameonywa kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo
hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, (National Steering Committee ) Eng. Rogatus
Mativila,wakati wa kufuatilia zoezi la Uhakiki lililoanza leo kwenye
Kata sita (6) Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Matavila, amesema kuwa
kumekuwepo na Walenga hewa sio jambo jema hata kidogo jambo ambalo limekuwa
likitolewa malalamiko sana.
“Uwepo
wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji aibu sana kwa viongozi wa
mikoa,wilaya na Halmashauri.Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote
.Kufanikiwa ama kutofanikiwa kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimo
nnitakavyotumia kujua kama mastahili kuendelea na nafasi mlizonazo au la.
Siwatishi lakini huo ndio ukweli’’ Amesema Mativila.
Amesema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa , walengwa
wa mpango wa kunusuru kaya maskini watahakikiwa kwa kuondolewa au kuingizwa
katika mpango kwa kufuata vigezo vilivyowekwa a serikali.
Mativila,
amesema kuwa Uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu ni muhimu katika kusimamia
zoezi la uhakiki wa Walengwa wa Mpango
wa TASAF ambao utasaidia kupata Takwimu sahihi za wanufaika Halisi
ndani ya Manispaa ya Morogoro.
Amesema
kuwa, Mkazo mkubwa katika Kipindi cha
Pili utawekwa katika kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye Mpango kufanya
kazi ili kuongeza kipato na kuhakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na
kuboreshwa na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa
elimu na afya.
Aidha,
amesema Pamoja na hayo tathimini ya serikali ya utekelezaji wa TASAF kipindi
cha kwanza awamu ya tatu inaonyesha umaskini nchini umepunngua kwa asilimia 10
kwa mahitaji ya msingi na umaskini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa
kaya maskini sana nchini.
Amewasisitiza
Viongozi na Maafisa Waandikishaji Kaya kufanya kazi kwa uadilifu na
weredi wakati wa utekelezaji wa Zoezi hili kama maagizo yaliivyotolewa na
Mh Rais katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili kuhusu uwepo wa kaya hewa.
“Nanukuu. “
Uwepo wa kaya hewa katika maeneo ya utekelezaji ni aibu sana kwa viongozi wa
Mikoa, Wilaya na Halmashauri. Nitoe wito kwa wahusika wote kusimamia vizuri
mradi huu. Serikali haitakuwa na huruma kwa mtu yeyote. Kufanikiwa ama kutofanikiwa
kwenye maeneo yenu itakuwa mojawapo ya vipimo nitakavyotumia kujua kama
mnastahili kuendelea na nafasi mlizonazo au la. Siwatishi lakini huo ndio
ukweli” mwisho wa kunukuu.
Mwisho, amewakumbusha wananchi wote kuchukua tahadhari
ya ugonjwa hatari wa COVID-19 ili kuepuka Mikusanyiko
isiyoyalazima, kuvaa barakoa, kuepuka kushikana mikono na
kunawa mikono kwa sabuni kwa kutumia maji safi yanayotiririka pamoja na
kutumia vitakasa mikono.
Post a Comment