DC MSULWA ATAKA MAONESHO YA NANE NANE YAWASAIDIE WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUONGEZA TIJA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI.
Ukaguzi wa Asili ya Milima ya Uluguru. |
Ukaguzi wa Bustani ya Jikoni ambayo inatumia mabaki ya vyakula . Zao la Red Cabbage linalostawishwa katika Shamba darasa. |
Ukaguzi wa Kilimo cha Greenhouse ambapo kumestawishwa nyana pamoja na Pilipili hoho. |
Kilimo cha Mpunga. |
MKUU
wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, ameziomba Halmashauri zote mbili
Morogoro Vijijini pamoja na Manispaa ya Morogoro kuhakikisha kwamba Maonesho ya Kilimo na Mifugo (Nane Nane) katika
Wilaya ya Morogoro yanawasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kiasi ili kuwawezesha
kubadili shughuli zao na kuzifanya kuwa na tija inayoridhisha.
Hayo
ameyazungumza leo Julai 07, 2020, wakati wa ziara ya kukagua na kutembelea vipando vya Shamba darasa la Manispaa ya
Morogoro pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikiwa ni kuangalia namna ya
maandalizi yanavyoendelea katika kuelekea katika maadhimisho hayo ya Kanda ya
Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agosti 1-8,2020 Mkoani Morogoro.
Akizungumza
na waandishi wa habari, DC Msulwa, amesema Maonesho ya Nane Nane yamekuwepo kwa miaka
mingi maeneo mbalimbali ya nchi katika Kanda mbalimbali na ukiyatembelea
utakutana na vitu vya kuvutia sana hususani Teknolojia na mbinu bora za
uzalishaji kilimo na mifugo ambazo zinauwezo wa kuleta tija kubwa lakini bado
changamoto kubwa mambo yote bora na mazuri yanayopatikana kwenye Maonesho bado
hayajaweza kumfikia mkulima kwenye ngazi za msingi.
Amesema
, kuwa unaweza kwenda maeneo ya
wakulima wenyewe ukashangaa kukuta mkulima analima kilimo cha kienyeji ambacho
hakina manufaa.
“Teknolojia inayooneshwa
kwenye Maonesho haya bado haijaweza kuwafikia wakulima na wafugaji wetu kwenye
vijiji vyao wanapoendeshea shughuli zao za kilimo na mifugo, lakini teknolojia
na ubunifu unaopatikana kwenye Maonesho haya unahitaji kuwafikia wakulima wa
chini kabisa, maana tusijekuwa tunaandaa maonehso haya kwa ajili ya tabaka la
watu wenye nacho tukawasahau wale wa hali ya chini ambao ndio wanaojihusisha na
kilimo na kuendesha maisha yao" Amesema DC Msulwa .
Aidha,
ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika
kuhakikisha Mashamba darasa yote ya halmashauri zote mbili vinakuwa vituo vya kudumu na wakati wote wataalamu wa kilimo na
mifugo wawepo kituoni hapo kipindi chote cha mwaka wakisimamia shughuli za
kilimo na mifugo kituoni hapo na Halmashauri zote zilete Wakulima na Wafugaji wao kujifunza na
kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za uzalishaji
.
Hata
hivyo, ameziagiza Halmashauri zote mbili ,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wanaounga mkono shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi waone namna wanavyoweza
kuifikisha kwa wakulima na wafugaji wetu elimu inayopatikana kwenye Shamba
darasa .
Mwisho, amewaomba wananchi ndani ya Wilaya ya Morogoro na nje ya
Wilaya hususani wakulima, wafugaji na
wavuvi kutembelea Maonesho hayo kwa wingi katika Shamba darasa ya Wilaya ya
,Morogoro kwa kuwa mambo mazuri
yakujifunza yapo mengi kubwa likiwa jinsi Teknolojia na mbinu bora za kuongeza
tija ya uzalishaji mazao ya kilimo na mifugo.
Naye
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka waangalizi wa
Shamba darasa kutumia muda ulipo kukimbiza na na maandalizi ili waweze kufanya
vizuri katika ngazi ya Kanda ya Mashariki.
“Niwaombe
Maafisa Mifugo na Kilimo ngazi zote waongeze nguvu na waangalie maeneo haya kwa
jicho la tatu, muda sio rafiki sana , tuna wiki 3 za maandalizi, tuhakikishe
kila kinachotakiwa kimefanyika , Maonesho haya yapo ndani ya Manispa yetu na
Wilaya yetu hatuna sababu za kufeli, naamni tukishirkiana kitimu na tukaongeza
ubunifu tutashinda vigezo vyote vipo ndani ya uwezo wetu”Amesema Lukuba.
Kwa
upande wa Afisa Kilimo Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, amesema maandalizi
yanaendelea vizuri ambapo washiriki wakuu ni pamoja na wakulima, wawakilishi wa
wakala wa makapuni ya pembejeo, wawakilishi wa wasindikaji wa mazo
mbalimbali, wawakilishi wa kampuni za umwagiliaji, wawakilishi wa kampuni za
dhana za kilimo pamoja na Idara mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro.
Aidha,
amesema miongoni mwa bidhaa zitakadhooneshwa ndani ya banda ni pamoja na mazao
mbalimbali yanayozalishwa na wakulima, bidhaa mbalimbali zinazosindikwa na
wakulima na wadau, shughuli za vyama vya Ushirika, shughuli za mawakala wa
kampuni za pembejeo, shughuli mbalimbali za Idara za Halamshauri, shughuli
mbalimbali za vikundi vya Vijana na Wakina mama, shughuli za kongano la nguo na
shughuli za wazalishaji wa miche ya maua na matunda.
Post a Comment