WANAWAKE WATAKIWA KUJIAMINI
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Jafari Makupula, akimkabidhi Cheti Bi, Yustina Wilbrod Mutafungwa (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wildina Foundation, wakati wa Kongamano la mfano la Wanawake lililoandaliwa na Ladiestalk Tanzania chini ya Mkurugenzi wa Taasisis hiyo Salome Sengo (katikati).
WANAWAKE nchini wametakiwa kujitambua ili waweze kupambana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo maeneo ya kazi na katika Jamii zinazowazunguka.
Hayo yamesema hivi karibuni na Mkurugenzi wa Ladiestalk Tanzania, Salome Sengo wakati wa Kongamano kubwa la kihistoria la Wanawake lililofanyika katika Ukumbi wa Savoy Hotel Manispaa ya Morogoro.
Sengo, amesema ni wajibu wa wanawake wenyewe kujua haki zao maeneo ya kazi pamoja na kutafuta fursa mbalimbali ikiwemo elimu ya ujasiriamali, Nguvu ya Uthubutu ndani ya Mabinti, Umuhimu wa Maamuzi chanya kwa Mabinti pamoja na jinsi ya kutumia kipaji na kukigeuza mtaji .
"' Wanawake wanatakiwa kujiamini na kutojisikia wanyonge kwa kujenga kujiamini na kufuata taratibu za kazi kama zinavyoelekeza katika kutimiza wajibu wao, lakini lazima wajitambue wao ni nani na wana mchango gani kwa Taifa na Jamii inayowazunguka, tumeitana hapa tunaamini baada ya Kongamano hili kila Mwanamke, Mabinti watasimama katika nafasi zao kama moja ya zao la uzalishaji na ukuzaji wa Uchumi kwani Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt John Pombe Magufuli imewaamini sana Wananwake katika kuwapatia nafasi mbalimbali za Uongozi""Amesema Sengo.
Mwisho katika Kongamano hilo, ilishuhudiwa Viongozi wakipatiwa vyeti vya utambuzi wa heshima kwa kutambua umuhimu wao katika kutetea masilahi ya Wanawake pamoja na kuwalinda na kuwatetea Watoto wakike katika upatikanaji wa haki zao.
Post a Comment