WAZAZI WASHAURIWA KUCHANGIA CHAKULA CHA WATOTO WAKIWA SHULENI
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Dr Janeth Barongo akikagua Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Waalimu |
WAZAZI wameshauriwa kuwa na desturi ya kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao mashuleni ili kuongeza kiwango cha ufaulu kwani watoto wengi wamekuwa wakifeli kutokana na utoro.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Dr Janeth Barongo, leo Julai 08,2020, wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ya kukagua Ujenzi wa madarsa 2 pamoja na Jengo la Ofisi ya Waalimu katika Shule ya Sekondari SUA iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Dr Barongo, amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikizikabili shule nyingi ni kutokana na wazazi kutochangia fedha kwa ajili ya chakula cha mchana kwa watoto wao hali ambayo huchangia kuwepo kwa utoro kwa watoto ambao hawali mashuleni.
Amesema kuwa kutokana na baadhi ya wazazi wengi kutokuwa na mwamko wa kuchangia chakula mashuleni, kumekuwa kukichangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kuwepo kwa division ziro shuleni hapo, hivyo amewaomba wazazi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya elimu ya watoto wao kwa kuchangia fedha kwa ajili ya chakula ili watoto waweze kusoma kwa utulivu.
"Kwa kweli uwepo wa baadhi ya wazazi wengi kutochangia chakula cha mchana kwa ajili ya watoto wao ndio wamekuwa wakichangia shule yetu kupata wanafunzi wenye division ziro, kwani wengi wa wanafunzi wanaopata ziro na wale ambao hawali chakula cha mchana hapa shuleni, hivyo tunawaomba sana wazazi wachangie chakula cha watoto ili tuhakikishe tunafuta division ziro."Amesema Dr Barongo.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya SUA , Mwl. Festo Kayombo, amesema kuwa kuna mambo mengi yanayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika Shule za Msingi na Sekondari ikiwemo Wanafunzi kutokupata chakula cha mchana mashuleni hali inayowafanya watoto kutofutilia masomo ipasavyo.
""Tumepokea wito kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa la kuwataka wazazi kuchangia cha mchana cha Wanafunzi, upande wetu tumeshawaita wazazi waweze kuchangia ambapo tumekubariana tarehe 09,2020 siku ya Alhamisi chakula kitaanza kuliwa shuleni kwa wale waliochangia wa awali wakati tukiendelea kupanga bajeti ya wengine wanaoendelea kuchangia , jambo ambalo litasaidia sana watoto wetu kuweza kusoma kwa umakini wakiwa wameshiba na wakaelewa vipindi darasani wakiwa wameshiba
Post a Comment