DC MSULWA ATAKA KERO ZA WANANCHI ZITATULIWE KWA WAKATI.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa kusikiliza kero za Wananchi. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe.
Bakari Msulwa, amewataka Watendaji kutatua kero za wananchi kwa wakati badala
ya kuendelea kusubiri ziara za viongozi.
Kauli hiyo ameitoa jana , Julai 16, 2020
katika Mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi uliofanyika kwenye
viwanja vya Shule ya Msingi K. Ndege Manispaa ya Morogoro.
Msulwa, alisema ziara hiyo ya Kata
kwa Kata imelenga kupunguza kama si kumaliza
kabisa kero za Wananchi.
Alisema kuwa kutokana na msimamo huo
wa kisheria na kutokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe.
Dkt John Pombe Magufuli, katika kutatua kero za wananchi, suala la utatuzi wa
kero za wananchi halitakiwi kuendelea kusubiri ziara za viongozi, badala yake,
kero hizo zitatuliwe kwenye ngazi zinazohusika na zitatuliwe kwa wakati.
“Tumefika hapa lakini tulichobaini
kuwa kero nyingi za Wananchi hazitatuliwi, hii ni kutokana na kutofanyika kwa
mikutano kama inavyotakiwa kisheria na Viongozi wa ngazi za chini , Watendaji hakikisheni kero
za wananchi wenu mnazitatua kikamilifu, msisubiri mpaka viongozi wa juu washuke
chini ,mmepewa mamlaka zote za kusimamia wananchi wenu, mnatakiwa mjiwekee
utaratibu wa kuwa karibu zaidi na wananchi kwa kuwafuata katika Kata zao na kufanya
mikutano maalum ya kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao na kuzitatua
papo kwa papo” Amesema DC Msulwa.
Aidha, alisema kuwa migogoro mingi na
kero nyingi zinasababishwa na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji ambao
wamepewa dhamana ya kuwaongoza wananchi kwa kuwapatia maendeleo.
Alisema ,suala la kutotatua kero za
wananchi katika ngazi ya Serikali za Mitaa ni kinyume na dhamira ya Serikali ya
kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi ambalo pia ni kinyume na msimamo wa
Ibara ya 146 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Madhumuni ya kuwapo Serikali za
Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi na vyombo vya Serikali za Mitaa
vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika
mpango wa shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika Serikali zao na nchi kwa
ujumla.”
“Nawasihi viongozi na Wataalamu wa Halmashauri ,
tembeleeni katika Kata na vijijini na mtatue kero za wananchi huko, lakini hakikisheni mikutano ya mitaa na Vijiji
iliyowekwa kwa mujibu wa sheria inafanyika na maazimio yake yanafika kwenye
vikao halali vya maamuzi, haiwezekani kuwaacha wananchi wanateseka harafu wewe
unajiita mtendaji, kuna kero zinatakiwa kweli Mkuu wa Nchi Mhe. Rais wetu
azitatua lakini sio kwa hizi ndogondogo ambazo tunaweza kuzitatua wenyewe tena
kwa ngazi za chini kabisa kwa kuwa Serikali yetu imeweka utaratibu wa
kiutawala kwa kila ngazi” Ameongeza DC Msulwa.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya
Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka watendaji wa kata, na mitaa kuitisha mikutano ya kisheria ya Mitaa na kata na mitaa
na kusoma taarifa za mapato na matumizi ya miradi ya maendeleo katika maeneo
yao.
“”Sisi tupo hapa kusikiliza kero za wananachi,
tumeona wapo wengine wanashindwa kufika katika Ofisi zetu aidha kwa kukosa muda
au nauli, lakini niwaombe Viongozi na Watendaji wa Mitaa na Kata jengeni utamaduni wa kuwatembelea wananchi katika
Mitaa yao na kusikiliza kero na
changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, hizi kero
ndogondogo tuzitatue sisi na Mhe. Rais wetu Dkt John Magufuli tumuachie zile kero
kubwa na kila mtu akifanya kazi kwa nafasi yake tutafanikiwa na wananchi wetu
watapata huduma nzuri zenye viwango zinazoendana na kasi ya Uongozi huu wa Awamu
ya tano” Amesema Lukuba.
Katika
ziara hiyo, DC Msulwa alipata muda wa kutembelea miradi ya Ujenzi ya Ofisi za
Kata ikiwamo Kata ya Chamwino, Mindu pamoja na Uwanja wa Taifa na kuhitimisha
na mkutano wa kusikiliza kero ambapo iWananchi wamepata fursa ya kuwasilisha kero
na malalamiko yao mbali mbali na Mkuu wa Wilaya kuzitatua papo hapo jambo
lililowafurahisha sana Wananchi hao.
Post a Comment