KAMATI YA SIASA CCM KATA YA TUNGI WAKOSHWA NA UTENDAJI WA MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Tungi, Zulfa Mkuya akitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro juu ya utendaji wake katika utoaji wa huduma kwa Wananchi. |
KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Tungi imepongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba anavyojitoa katika kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Manispaa ya Morogoro hususani Kata ya Tungi.
Pongezi
hizo zimetolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tungi, Zulfa
Mkuya, kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM
Kata ya Tungi , kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Choo cha Mfano cha Mtoto wa
Kike Shule ya Sekondari Tubuyu.
Akizitoa
pongezi hizo, amesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ameonesha uzalendo
katika kuhakikisha ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 hadi 2020, inatekelezwa kwa
vitendo kwa kutumia makusanyo yao ya Ndani, Fedha kutoka Serikli kuu pamoja na
Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.
‘” Manispaa
ya Morogoro hususani Mkurugenzi wetu kwakweli anaitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka
2015-2020, miradi iliyotekelezwa Manispaa yetu kwa kushirikiana na Baraza la
Madiwani ni mfano wa kuigwa na itakuwa alama na taswira inayoonekana kwa Wananchi.tunashuhudia
mifereji na sehemu korofi za barabara ndani ya Kata yetu ikifanyiwa kazi,
tumeona leo Magari ya kubebea takataka kufanya Mji safi na sasa uzinduzi wa Choo hiki
cha mfano tunaamini yapo mengi yanakuja kwetu kikubwa tuendelee kumpa
ushirikiano , ametuahidi kuwa barabara yetu ya Tungi kuanzia Julai ya mwaka huu muda na
wakati wowote itatengenezwa kwa kiwango cha lami hili ni jambo jema
litakalowasaidia Wanafunzi na wananchi kupata urahisi wa usafiri tunajivunia
kuwa na Kiongozi mchapakazi kama huyu Dada yangu Lukuba " Amesema Mkuya.
Aidha,
amebainisha kuwa thamani halisi ya fedha
imeonekana Katika miradi hiyo kwani mbali na kutumia fedha za ndani, Serikali
kuu na wadau, lakini pia kiasi kinachotumika katika ukamilishaji wake
vinaenda sambamba na ubora .
Mbali
na ujenzi wa barabara , amesema Kata ya Tungi imepokea fedha za miradi sio
chini ya Milioni 80 mpaka sasa , ambapo katika ujenzi wa Shule ya Msingi Tubuyu
mpaka sasa jumla la madarasa 3 yamekamilika na madarasa mawili yananyanyuliwa,
milioni 17 zimetolewa kwa ajili ya mradi wa Zahanati ya Tubuyu ambayo tayari
hatua ya uwekaji wa madirisha umefanyika, shilingi milioni 56 zimetolewa kwa
ajili ya mradi wa uchomaji wa nyama Choma katika mnada wa Ngómbe ambapo ujenzi
huo umeanza rasmi jana Juni 30, 2020 ambapo ifikapo maonyesho ya Nanenane
wananchi waweze kupata huduma hiyo.
Mwisho
amewaomba wananchi wa Manispaa ya Morogoro, Kata ya Tungi kuweza kuwachagua
Viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi watakaopewa ridhaa ya kuwakilisha
katika Uchaguzi wa Oktoba mwaka 2020 ikiwamo kura za Mhe. Rais, Wabunge na
Madiwani pamoja na Madiwani wa Viti Maalum.
Post a Comment