MAAFISA WAANDIKISHAJI WA TASAF WATAKIWA KUWA WAADILIFU WAKATI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA KAYA ZA WANUFAIKA WA TASAF.
Zoezi la uhakiki Kaya zilizo katika Mpango wa TASAF likiendelea. |
Walengwa wa TASAF wakiwa nje ya Ofisi ya Kata ya Kihonda Maghorofani katika uzinduzi rasmi wa zoezi la uhakiki wa Kaya zilizo katika Mpango wa TASAF. |
MAAFISA wawezeshaji wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kuwa waadilifu wakati wa zoezi la
uhakiki wa Kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF)
katika utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.
Hayo
yameelezwa leo Julai 22,2020 na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani TASAF Makao Makuu, CPA-Christopher Sanga,
wakati wa ufunguzi wa zoezi hilo la Uhakiki lililoanza leo kwenye Kata 6
Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Sanga, amewataka wawezeshaji hao kuwa makini wakati wa
kuhakiki taarifa za Walengwa ili kufanikisha zoezi la uhakiki wa kaya za
walengwa wa TASAF na kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya
kuwepo Walengwa hewa.
Aidha,
CPA Sanga, amewataka wawezeshaji hao ambao ni watumishi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro kuwa waaminifu na waadilifu wakati wa zoezi hilo.
“Hatua
hii ni muhimu sana kwetu . tunawaomba Maafisa wetu mmepewa kazi hii kwa
uaminifu tukiamini kwamba mtaitendea haki ili kuwapata walengwa halisi na
kuondoa dhana ya walengwa hewa, mfuate miongozo ,kanuni na taratibu
zilizowekwa na serikali ili kufanikisha zoezi hili limalizike kwa ufanisi wa
hali ya juu sana, mmeshapata mafunzo hatutegemei kwamba mtatuangusha fanyeni
kazi shirikianeni vyema na Wenyeviti wa Mitaa ambao wao ndio wenye wananchi hao
mitaani ili zoezi letu lifanikiwe “Amesema Sanga.
Sanga.
ameeleza kuwa Serikali iliamua kuendelea na kipindi cha pili
katika awamu ya tatu ya TASAF ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni
zipate usaidizi kwani katika kipindi cha kwanza cha TASAF awamu ya tatu,
idadi ya kaya zilizofikiwa ni sawa na 70 % ya Kaya zenye mazingira duni
nchini, hivyo kipindi cha pili cha TASAF
awamu ya tatu kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 Tanzania Bara na Wilaya
zote za Zanzibar ambapo jumla ya kaya milioni moja laki nne na nusu zenye
jumla ya watu zaidi ya milioni 7 kote Nchini zitafikiwa ikiwa ni ongezeko la
kaya laki tatu na nusu.
Amewatahadharisha
wawezeshaji hao
kufanya kazi kwa waadilifu kwani
wakienda kinyume kwani
watawajibishwa endapo itabainika uwepo wa Kaya zisizo na sifa katika eneo
walilofanya kazi .
Ikumbukwe
kwamba zoezi hilo la kuhakiki Kaya za
wanufaika wa TASAF limeanza leo Julai 22, 2020 katika Kata 6 za awali za
Manispaa ya Morogoro zikiwemo Kata ya Kihonda Maghorofani, Bigwa, Boma,
Chamwino, Kiwanja Cha Ndege pamoja na Kauzeni ambapo zoezi hilo litaendelea
tena hadi kuzifikia Kata zote 29 za Manispaa ya Morogoro.
Kabla
ya zoezi hili la Uhakiki wa Kaya za Wanufaika wa TASAF , kulikuwepo na Semina
ya Wawezeshaji ya kuwajengea Uwezo iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Julai
20-21, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Naye
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana,amesema zoezi hilo
limeanza kwa matumaini kwani hata idadi ya walengwa waliojitokeza imekuwa na
uwiano mzuri.
“”Zoezi
limeonyesha matumaini makubwa, hapa Kata ya Kihonda Maghorofani kuna jumla ya
Walengwa 61 lakini kwa idadi tunayoiona imeonesha kwamba mwitiko umekuwa mkubwa
sana , hata Kata ya Chamwino watu wameitika sana kikubwa niwaombe Wataalamu
wangu waendeshe zoezi hili kwa umakini sana hata kama kuna dosari zitajitokeza
zitakuwa ndogo ndogo ambazo naamini wakishrikiana vyema na Wenyeviti wa Mitaa
watazitatua bila wasiwasi” Amesema Katemana.
Katemana
amesema mpango wa kipindi cha Pili
cha Awamu ya Tatu ya TASAF Manispaa Morogoro utalenga jumla ya Walengwa 2793
katika Kata 29 ikiwamo Mitaa 164.
Ratiba ya Zoezi la Uhakiki ni kama ifuatavyo;
Na
|
KATA
|
TAREHE
|
1
|
KICHANGANI
|
23/07/2020
|
2
|
KILAKALA
|
23/07/2020
|
3
|
KINGOLWIRA
|
23/07/2020
|
4
|
LUHUNGO
|
23/07/2020
|
5
|
LUKOBE
|
23/07/2020
|
6
|
MAFIGA
|
23/07/2020
|
7
|
MAGADU
|
23/07/2020
|
8
|
MAZIMBU
|
23/07/2020
|
9
|
MBUYUNI
|
23/07/2020
|
10
|
MINDU
|
24/07/2020
|
11
|
MJI MKUU
|
24/07/2020
|
12
|
MJI MPYA
|
24/07/2020
|
13
|
MKUNDI
|
24/07/2020
|
14
|
MLIMANI
|
24/07/2020
|
15
|
MWEMBESONGO
|
24/07/2020
|
16
|
MZINGA
|
24/07/2020
|
17
|
SABASABA
|
24/07/2020
|
18
|
SULTAN AREA
|
24/07/2020
|
19
|
TUNGI
|
24/07/2020
|
20
|
UWANJA WA TAIFA
|
24/07/2020
|
21
|
MAFISA
|
24/07/2020
|
Post a Comment