Header Ads

WALENGWA WA TASAF MANISPAA MOROGORO WATAKIWA KIUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA ZOEZI LA UHAKIKI KAYA MASIKINI.






Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana akiongea na walengwa wa mfuko huo.



WALENGWA wa TASAF Manispaa ya Morogoro, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuhakiki na Uhuishaji wa Taarifa za Walengwa wa Kaya Masikini kwenye Kata zao.

Hayo yamezungumzwa  leo Julai 20,2020 na Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana, wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili awamu ya tatu na uhakiki wa Kaya zinazoshiriki kwenye mpango wa TASAF.

 ‘”Tumeshazindua mpango wa Kipindi cha Pili Awamu ya Tatu wa TASAF, niwaombe Walengwa wote zoezi hili la uhakiki na Uhuishaji wa taarifa za Walengwa  utaanza Julai 22,2020 Jumatano, niwaombe Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Mitaa, Kata muwahamasishe walengwa wajitokeze kwa wingi, wale amabao watakosa katika uhakiki watakuwa wamejiondoa wenyewe katika mpango huu” Amesema Katemana.

Katemana,  amesema mpango wa  kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF Manispaa Morogoro utalenga jumla ya Walengwa 2793 katika Kata 29 ikiwamo Mitaa 164.

Ratiba ya Zoezi la Uhakiki ni kama ifuatavyo;

Na
KATA
TAREHE
1
BIGWA
22/07/2020
2
BOMA
22/07/2020
3
CHAMWINO
22/07/2020
4
KIWANJA CHA NDEGE
22/07/2020
5
KIHONDA MAGOROFANI
22/07/2020
6
KAUZENI
22/07/2020



7
KICHANGANI
23/07/2020
8
KILAKALA
23/07/2020
9
KINGOLWIRA
23/07/2020
10
LUHUNGO
23/07/2020
11
LUKOBE
23/07/2020
12
MAFIGA
23/07/2020
13
MAGADU
23/07/2020
14
MAZIMBU
23/07/2020
15
MBUYUNI
23/07/2020



16
MINDU
24/07/2020
17
MJI MKUU
24/07/2020
18
MJI MPYA
24/07/2020
19
MKUNDI
24/07/2020
20
MLIMANI
24/07/2020
21
MWEMBESONGO
24/07/2020
22
MZINGA
24/07/2020
23
SABASABA
24/07/2020
24
SULTAN AREA
24/07/2020
25
TUNGI
24/07/2020
26
UWANJA WA TAIFA
24/07/2020
27
MAFISA
24/07/2020




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.