JUMLA YA SHILINGI MILIONI 55 ZATUMIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA LUHUNGO MANISPAA YA MOROGORO.
Muonekano wa Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luhungo. |
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Kata ya Luhungo . |
Choo cha kisasa kilichpo Kata ya Luhungo . Muonekano wa ndani wa Choo. |
JUMLA ya Shilingi milioni 55 zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza
na Chombo huru , Afisa Mtendaji Kata ya Luhungo , Said Rashid Maleta leo
Julai 02, 2020, amesema fedha hizo zimetolewa na Halmashauri ya Manispaa ya
Morogoro kupitia mapato ya ndani.
Maleta,
amesema kuwa Manispaa ya Morogoro katika kuunga
mkono jitihada za wananchi , iliamua kutekeleza miradi ya maendeleo kwa
kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo ilitengea Kata hiyo kutoka katika
makusanyo ya mapato ya ndani jumla ya shilingi milioni 55 katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa Ofisi ya Kata milioni 20 , Ujenzi wa Nyumba ya
Mwalimu milioni 25, pamoja na Ujenzi
Choo cha kisasa kilichogharimu shilingi milioni 10.
Aidha, Mtendaji wa Kata ya Luhungo,
amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba, kwa jitihada
zake za kusukuma gurudumu la maendeleo katika Kata hiyo la Luhungo.
Licha ya kumshukuru
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro lakini ametoa pongezi Baraza la Madiwnai la Mnaispaa ya
Morogoro, aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo
Mhe. Rajabu Mizambwa , Uongozi wa Kata pamoja na Wananchi wa Kata hiyo kwa
kujitoa kwao katika kuchangia masuala ya Maendeleo.
Mwisho ,amesema mradi wa Choo
na Nyumba ya Mwalimu imeshakamilka wakati huohuo wakisubiria fedha nyengine kwa
ajili ya kukamilisha mradi wa Jnego la Ofisi ya Kata.
Post a Comment