ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 722 ZATUMIKA KUNUNULIA MAGARI YA TAKATAKA MANISPAA YA MOROGORO.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Bakari Msulwa, (aliyevaa suti nyeusi) akikata utepe kuzindua rasmi magari yaliyonunuliwa
na Manispaa ya Morogoro pamoja na Magari ya usafishaji wa Mji kutoka Kampuni ya Kajenjere iliyopata dhabuni ya
kufanya kazi hiyo, (kulia ) Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba., Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro, Dr Janeth Barongo,Afisa utumishi Manispaa ya Morogoro Waziri Kombo.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, akitesti mitambo wakati
wa kukaguaa magari ya kisasa ya kufanya usafi yaliyonunuliwa na Manispaa ya
Morogoro.
Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro , Samweli Subi, (kushoto) akisoma taarifa ya ununuzi wa magari ya taka na taswira ya hali ya usafi Manispaa ya Morogoro mbele ya Mkuu wa Wilaya. |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa , katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya Kajenjere akipokea taarifa fupi kutoka kwa Mwakilishi wa Kmapuni hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Kajenjere wakiwa tayari kwa kazi za usafishaji wa Mji.
Magari ya kuzoela taka (Compactor) yakiwa eneo ambalo yatakuwa yana kaa baada ya shughuli za uzoaji wa taka kumalizika. Eneo hilo lipo jira na Ofisi ya Kata ya Mji Mkuu.
MKUU
wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amezindua magari manne (4) ya
kubebea takataka yenye thamani ya Shilingi milioni 722,890,731/= yaliyonunuliwa
na Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuweka Mji safi.
Zoezi
hilo la uzinduzi wa magari hayo limefanyika katika viwanja vya Ofisi ndogo za
Manispaa ya Morogoro ambapo hutumika
katika kuhifadhia magari (Yard) leo Julai 01, 2020.
Akizungumza
na Waandishi wa habari, amesema hiyo ni hatua kubwa ambayo sasa itakwenda
kusaidia kuondoa na kumaliza changamoto ya kuzagaa kwa takataka mitaani na
kuziingiza Dampo.
Sambamba
na uzinduzi wa Magari hayo ya taka lakini tukio hilo limeambatana na mapokezi
ya Magari ya kuzolea takataka (Compactor 5) na gari la kisasa la kusafisha barabara, kunyonya mchanga pamoja na kusafisha barabara kwa maji (Sweeper Loader) kutoka Kampuni ya Kajenjere.
Licha ya ununuzi wa magari hayo, DC
Msulwa, ameipongeza Manispaa ya Morogoro kwa kufanikiwa kuingia mkataba na
kampuni ya Kajenjere wa kufanya usafi
katika kata 12 za Manispaa ya Morogoro kwa kuwa Kampuni ya Kajenjere ina vifaa na magari ya kisasa, ambayo anaamini
yatafanikisha lengo la kuweka Mji kuwa safi.
Kikubwa ameomba Wananchi watoe ushirikiano na washiriki katika kufanya usafi katika maeoneo yao na kulipa ada ya
uzoaji wa taka ili kuwezesha shughuli hiyo kufanyika kwa ufanisi mkubwa katika
kuepukana na magojwa ya milipuko.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameshukuru Mhe. Rais
Dkt John Pombe Magufuli kwa kuipatia Manispaa ya Morogoro Shilingi Milioni 722,
890,731/= za kununulia magari manne ya taka.
Kwa upande wa Afisa Mazingira Manispaa ya Morogoro, Samweli Subi,amesema
kuwa Manispaa ya Morogoro imedhamiria kufanya usafi na kuwa mfano wa kuigwa
miongoni mwa Halmashauri za mkoa wa
Morogoro hadi ngazi ya Taifa.
Subi, amesema kuwa kwa sasa
kampuni ya Kajenjere itaanza kazi ya usafi katika kata za Mji Mkuu, Mafiga,
Sabasaba, Kingo, Mwembesongo, Mji Mpya, Kilakala, Kichangani,Mafisa,K. Ndege,
U/Taifa, pamoja na Kihonda Maghorofani.
Aidha, amesema kuwa, kiasi cha taka zinazozalishwa kwa siku ni tani 231
na uwezo wa kuzoa taka kuzipeleka dampo ni asilimia 79 sawa na tani 180.
Amesema zoezi la usafishaji wa mji linakabiriwa na changamoto ya
ongezeko la biashara ndogondogo katika maeneo yasiyo rasmi ambapo biashara hizo
zinapelekea utupwaji wa taka hovyo ikiwamo kandokando ya barabara , kwenye
mifereji ya maji ya mvua, maeneo ya wazi, majengo ambayo hayajakamilika kujengwa
pamoja na maeneo ambayo viwanja havijaendelezwa.
‘Tumeamua kutafuta mdhabuni mwenye uwezo wa kuwa na magari ya kutoa
huduma ya usafi katika Kata 12 na masoko 4 yenye uzalishaji mkubwa wa taka na tumevipa vikundi vya usafi kwenye Kata 17 zenye uzalishaji mdogo wa taka, changamoto
kubwa iliyotufanya tutafute mdhabuni ni baada ya
kuona vikundi vyetu vya taka havina uwezo wa kuwa na magari ya taka na kupeleka
taka kutoondolewa kwenye makazi na maeneo ya biashara kwa wakati na kusababisha
kero kwa wananchi na na baadhi ya wnaanchi kutolipa ada kwa wakati, ” Amesema
Subi.
Naye Msimamizi wa ukusanyaji wa takataka kutoka Kampuni ya Kajenjere,
Oswini Mwaitete, amesema lengo la kampuni yao ni kuhakikisha Manispaa ya
Morogoro inakuwa safi akiamini kuwa
baada ya miezi michache wananchi wataanza kuona utofauti.
Mwaitete, amesema kuwa Kampuni yao wana vifaa vya kisasa ikiwamo gari la
kisasa la kusafisha barabara, kunyonya mchanga na hata kusafisha barabara kwa
maji.
Post a Comment