DC Msulwa afufua matumaini ya kuunganishiwa umeme mkazi wa Kata Kingolwira Manispaa Morogoro baada ya kuteseka kwa muda wa miaka 5.
Nyumba ya Bi Joyce Macha, iliyopo ndani ya eneo la Shule ya Sekondari Iyula Malaika. Shamba la Bi Joyce Macha, lililopo ndani ya eneo la Shule ya Sekondari Iyula Malaika. |
Mwenyekiti wa Wamachinga Manispaa ya Morogoro , Ndug Faustine Alimas ,akitambulisha Uongozi wake katika kikao cha Mkuu wa Wilaya. |
MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amefufua
matumani ya Mkazi wa Mtaa wa Shule Kata ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro, Bi.
Joyce Macha , baada ya kuagiza Shirika la Umeme TANESCO kumunganishia Umeme mkazi huyo.
Hayo yamejiri leo Julai 18,2020, wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kutatua kero za wananchi ambapo ameagiza Shirika la Umeme TANESCO Manispaa ya Morogoro kufikia kesho Julai 19,2020 kazi ya kuanza kuunganisha
huduma ya umeme kwa mkazi huyo iwe imeshaanza.
Kauli hiyo ameitoa kufuatia mgogoro uliodumu kwa takribani
miaka 5 tangia mwaka 2014 kati ya Bi. Joyce Macha na mmiliki wa Shule ya Sekondari
Iyula Malaika iliyopo Kata ya Kingolwira ambaye aliendelea kushikiria msimamo wake wa
kukataa mwananchi huyo kuwekewa huduma ya umeme kwa kile alichodai kwamba mkazi huyo
alivamia katika eneo lake la Shule.
“”Haiwezekani mtu akanyimwa huduma ya umeme, kila raia ana
haki za kupata huduma bila kuvunja sheria za nchi, umeme uwekwe kwa mwananchi yeyote anaehitaji na mwenye uwezo wa kulipia
gharama za kuunganisha hata kama nyumba yake ni ya udongo na kuezekwa kwa nyasi,
lakini cha kusikitisha hata kama eneo hilo lingekuwa na kesi kubwa kiasi
gani lazima mtu apate huduma kama haki yake ya msingi , kesi hii imeshamalizika , Kamishina ardhi alishatoa hukumu , na eneo hilo limebaki mali ya kimila na
hakuna mwenye eneo hivyo mama huyu anatakiwa apate huduma haraka iwezekanvyo ili
maisha yake yaende na maisha ya utoaji wa elimu yaende bila kuathiri shughuli za mtu
yeyote” Amesema DC Msulwa.
Kwa upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth
John, amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kulivalia njuga swala hilo na hatimaye
haki imepatikana.
“”Huu ni mgogoro wa muda mrefu, umekuwa ukitusumbua sana ,
lakini Mkuu wetu wa Wilaya amefika hapa amejionea lakini tunampongeza sana kwa
vile ametoa maelekezo mazuri kutokana na hukumu ya Kamishina wa ardhi alivyoitoa,
kikubwa familia hizi ziishi vizuri kwani wao bado ni majirani wanatakiwa
washirikiane badala ya kuleteana chuki” Amesema
DAS Ruth.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba,
amemuagiza Afisa ardhi wa Manispaa ya morogoro kuandaa michoro ya hapo ili wale
wenye maeneo waweze kuyamiliki kihalali kufuatia maeneo hayo michoro yao
kufutwa.
Afisa Ardhi Manispaa ya Morogoro, Gisbert Msemwa, amesema
muda wowote wataanza utaratibu wa kuandaa michoro mipya ili maeneno hayo yaweze
kupimwa na wenye maeneo waweze kuwa na hati miliki ya ardhi kwani mpaka sasa
maeneo hayo ni ya kimila na hakuna mwenye umiliki wa ardhi.
“Hii kesi ya muda mrefu, lakini eleo imepatiwa ufumbuzi,
sisi kazi yetu kuanda michoro na kama wenye maeneo watapenda tuendelee nao
kupima tutayapima au wanaweza kuwapata watu wengine lakini kubwa zaidi hata
eneno hili halikuwa limekusudiwa kuwa Shule bali eneo hili lilikuwa shamba
hivyo hakuna taarifa ya kubadili
matumizi ya eneo hili tuliyonayo, kwahiyo kuyapima na kuweka michoro kutampa fursa mmiliki wa Shule hii kubadilisha matumizi ya ardhi na kupata kibali
rasmi cha ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kutoka shamba kuja eneo a huduma
ya shule””Amesema Msemwa.
Mkazi wa eneo hilo la Shule, Bi Joyce Macha, amemhukuru Mkuu wa Wilaya , Katibu Tawala, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro pamoja na Idara ya ardhi kwa kulipambania suala lake na hatimaye kuipata haki yake aliyokuwa akiisubiria kwa muda mrefu.
Amesema sasa ameanza kupata matumaini mapya ya kupata hudma ya umeme kwa muda mraefu na ameahidi kuendelea kushirikiana na majirani zake waliopo katika eneno hilo la shule kwani bado maisha yanaendelea.
Katika hatua nyengine DC Msulwa, , ameuomba Uongozi wa Machinga Manispaa
ya Morogoro kufanya kazi kwa uwaledi katika kuwaongoza wamachinga ili waweze
kujipanga vizuri na kufanya biashara zao katika maeneo yaliyo salama.
"Nimesikia hapa kuna watu wanajiita wazawa na wandewa, wanawatoza watu pesa kuwakodishia maeneo , tabia hiyo ife mara moja, mtu akiwa na kitambulisho cha Wajasiriamali haruhusiwi kutozwa hela, sasa chukueni hizo hela za wandewa ipo siku mtachukua hela za wandewa wenzenu bila kujijua na mtaangukia mahala pabaya,ridhikeni na vipato vyenu pesa hizi mnazochukua za moto " Ameongeza DC Msulwa.
Pia ameagiza kuanzia mnada ujao wafanyabiashara wote wanaofanya
baishara katika maeneo ya Shule ya Msingi Kikundi, Ofisi ya Kata ya Sultan Area pamoja na Kituo cha Polisi Kikundi kuondoka maeneo hayo na wafanye
biashara eneo ambalo wamepangiwa na kamati yake ya kuandaa maeneo inayoongozwa
na Afisa Tarafa Manispaa ya Morogoro, Wenyeviti wa Mitaa pamoja na Uongozi wa
Wamachinga Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment