MANISPAA MOROGORO YAZINDUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI KWA KAYA ZINAZOSHIRIKI KWENYE MPANGO WA TASAF KIPINDI CHA PILI AWAMU YA TATU.
Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana, (aliyevaa baluzi nyeupe) akifuatilia kwa makini mafunzo ya Mpango wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu . |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro, imezindua mafunzo ya
wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili awamu ya tatu na uhakiki wa
Kaya zinazoshiriki kwenye mpango wa TASAF.
Mafunzo hayo yamezinduliwa leo Julai 20,2020 na Mkurugenzi
wa Ukaguzi wa ndani TASAF Makao Makuu, CPA-Christopher Sanga, kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa Manispaa.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Sanga, amesema mafunzo
hayo ni kujenga uwelewa wa pamoja na namna zoezi hili la uhakiki wa walengwa ambayo ni ya kwanza katika utekelezaji wa
kipindi cha pili cha Awamu ya tatu ya TASAF ambacho kilizinduliwa na Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Februali 2020.
Sanga , amesema tathimini ya kipindi cha kwanza cha Awamu ya
Tatu TASAF inaonyesha kwamba mpango wa kunusuru Kaya zinazoshiriki kwenye
mpango wa TASAF umechangia kwa kiasi kufikiwa azma ya Serikali ya kupunguza
umasikini nchini.
Amesema utekelezaji wa kunusuru mpango wa Kaya Masikini pia
umewezesha Kaya za Walengwa kujikita kwenye shughuli za kukuza kipato na
kijiimarisha kiuchumi ikiwemo Ufugaji, uvuvi, kilimo, na biashara ndogondogo.
Aidha, amesema pamoja na mafanikio hayo Vijiji/Mitaa/ Shehia
zilizofikiwa katika kipindi cha kwanza ni asilimia 70% ya Vijiji/Sheria/ Shehia
vyote nchini hivyo bado kuna wananchi wanaoishi katika hali duni kwenye maeneo
ambayo hayakufikiwa.
“Wakati wa uzinduzi wa kipindi hiki cha pili, Mhe. Rais Dkt
John Pombe Magufuli, aliagiza kwamba kabla ya shughuli zozote za kipindi cha
pili kuanza, uhakiki wa walengwa ufanyike kote nchini ili kuondoa Kaya za
walengwa ambazo zimepoteza sifa, mtakumbuka hapo nyuma kumekuwa na malalamiko
mengi kuhusu mpango kuwa na watu wasiostahili wakiwemo watu wasio kuwa
masikini, Viongozi, orodha ya walengwa kuwa na watu waliohama au waliofariki
ambao hao wote waliitwa walengwa hewa, ili kutekeleza agizo la Mhe. Rais na pia
kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya kuwemo walengwa hewa, tutaanza
uboreshaji kwa kusafisha daftari leo la walengwa”Amesema CPA Sanga.
Amesema kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF ,kitafikia
Kaya Milioni moja na laki nne na nusu zenye jumla ya watu zaidi ya Milioni 7
Kote nchini hii ikiwa ni nyongeza ya Kaya laki tatu na nusu ambapo mkazo mkubwa
utakuwa ni kuwezesha Kaya zitakazoandikishwa kwenye mpango kufanya kazi kufanya
kazi ili kuongeza kipato.
‘”Tunataka kuwa na orodha Halisi ya Walengwa kwenye Masijala
ya Kaya za Walengwa , Kaya ambayo haikufika kuchukua malipo yake mara mbili
mfululizo Kaya hizo zote lazima ziondolewe” Ameongeza CPA Sanga.
Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii- TASAF, (National Steering Committee ) Eng. Rogatus Mativila, amewataka Viongozi
wafanye kazi kwa uadilifu ili wafikie
malengo ya Serikali kupitia kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF ya
kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji
wa uchumi ukiwemo ule wa Viwanda ambayo ni agenda muhimu ya Serikali.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,
ameupongeza Uongozi wa TASAF Mkao Makuu kwa kuzindua mpango huo ambao unaongeza
na kuboresha ili kutoa huduma za jamii na kuendeleza rasilimali Watoto hususani
katika upatikanaji wa elimu na Afya.
Kwa upande wa Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro,
Feliciana Katemana, amesema mpango huo wa kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu , utawezesha
Kaya zote zinazoishi katika Mazingira duni zipate usaidizi wa Serikali kupitia
TASAF kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umasikini.
Katemana amesema mpango wa
kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF Manispaa Morogoro umelenga kuwafikia jumla ya Walengwa 2793 katika Kata 29 ikiwamo Mitaa 164.
Post a Comment