Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro aahidi ushirikiano Jukwaa la Wanawake Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, (kulia), Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe (kushoto ya mkurugenzi. |
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema ataendelea kushirikina na Uongozi wa Jukwaa la Wanawake Manispaa ya Morogoro katika kuhakikisha wanasogeza huduma karibu kwa wanavikundi wanaowaongoza.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 09, 2020 Ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na Uongozi wa Jukwa hilo na kumpongeza kwa kazi anazozifanya za kuwahudumia wananchi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na kusimamia vyema miradi ya Maendeleo.
Lukuba, amesema amefurahishwa saana na ujio wa Uongozi huo wa Jukwaa Ofisini kwake kwani tangia awasili Manispaa ya Morogoro hajawahi kupata ugeni kama huo Ofisini kwake.
'"Nimefurahishwa sana na ujio huu, tangia nifike hapa nilikuwa napata shida sana ya kuwafikia wakina mama kwa karibu lakini kwa ujio wao tunafungua ukurasa mpya , tunaamini hata ile mikopo tunayoitoa kwa Vikundi vyetu hususani wakina Mama Uongozi huu una msaada mkubwa katika usimamizi, endeleeni kupiga kazi, mikopo hii Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli, ameitoa kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi kujikwamua na maisha na kuondoa umasikini lakini kulifanya Taifa hili kuingia katika uchumi wa Kati ambapo tayari malengo hayo yameshatimia " Amesema Lukuba.
Aidha, amesema kuhusu changamoto zinazowakabili hususani suala la Ofisi, watashirikiana kuona wanapata Ofisi karibu na Mji ili waweze kusogeza huduma karibu kwa jamii na wananchama wao.
"Nimeona kuna suala la Ofisi limejitokeza, lakini nimewaelekeza wakutane na Meneja wa Stendi ya Mabasi Msamvu waone jinsi wanavyoweza kufanikisha ofisi na kuwa mjini tofauti na sasa ipo mbali jambo ambalo linachangia kutowafikia wanachama wao kwa urahisi, wamesema wanachangamoto ya pango lakini nimewaongezea kiasi cha Shilingi 110,000/= ili iwasaidie katika ulipaji wa pango la Ofisi, wamenipatia kanga kama zawadi nawashukuru sana na waomba wakina mama wengine tuendelee kuwaunga mkono wajasiriamali wetu wa ndani ili kunyanyua vipato vyao na kuweza kurudisha fedha za mikopo wanazopatiwa na Halmashauri" Ameongeza Lukuba.
Naye Mwenyekiti wa Jukwa la Wanawake Manispaa ya Morogoro, Bi Marry Kachale, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kwa kazi zinazofanyika huku wakimuahidi kumpa ushirikianao zaidi katika kuleta maendeleo .
Bi. Kachale, amesema ujio wo katika Ofisi ya Mkurugenzi ni ni pamoja na kujitambulisha kama Jukwaa la Wanawake Manispaa ya Morogoro, kutambulisha kazi zao wanazozifanya, na kumpongeza Mkurugenzi kwa kazi anazozifanya katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Amesema kwa kutambua umuhimu na majukumu ya Mkurugenzi wataendelee kumpa ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha wanasimamia vyema vikundi vya wakina Mama vilivyopewa mikopo ili virudishe kwa wakati.
Post a Comment