Header Ads

MRADI WA STENDI YA DALADALA KALOLENI WAFIKIA ASILIMIA 75 , MKANDARASI ATAKIWA KUONGEZA KASI YA UJENZI.


Mfuatiliaji na uthaminishaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za   uboreshaji Miji ( Urban Local Government Strengthening Program (ULGSP) , Rubeni Emilly (kulia) akiwa na Msimamizi wa Ujenzi wa Stendi ya Daladala Kaloleni Peter Salvatory wakikagua ujenzi unavyoendelea.


Mfuatiliaji na uthaminishaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za   uboreshaji Miji ( Urban Local Government Strengthening Program (ULGSP) , Rubeni Emilly Rubeni Emilly , amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa Stendi  ya Daladala Kaloleni , unaosimamiwa na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ujenzi ya Nandhra , kuhakikisha mradi huo unakwenda kwa  mkasi kubwa.
Hayo ameyasema leo,Julai 09,2020  mbele ya waandishi wa habari, mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rubeni , amesema kasi inatakiwa kuongezeka ,  hivyo amemtaka mkanadarasi kufanya kazi usiku mchana kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.
Amesema lengo la kutekeleza mradi huo wa Stendi ya Daladala unaogharimu Shilingi  Milioni 644, ndani ya Manispaa ya Morogoro  , umetokana na  hali halisi ya  Stendi  iliyopo katikati ya Mji kuzidiwa na wingi wa watu, wingi wa magari na ukuaji wa mji.
" Mkandarasi kasi ya mradi bado, tunataka matokeo, tunataka mradi ukamilike, hizi pesa tunazotumia ni za watu na ifikapo mwezi Julai mwishoni 2020 muwe mmetukabidhi mradi huu,  fanyeni kazi kwa spidi kubwa na pale mnapoona mnakwama mtushirikishe kwa haraka tuone namna gani tunaweza  kusaidiana ili ujenzi huu ukamilike na ulete tija kwa wananchi na kutoa huduma bora" Amesema Rubeni.
Naye Mhandisi wa mradi kutoka Kampuni ya Ujenzi Nandhra, Eng. Ramadhani Yasini,  , amesema ujenzi huo mpaka sasa umefikia asilimia 75.
 ""Mwisho  mwa mwezi huu wa saba 2020, tutakuwa tumeukamilisha lakini tumeomba kuongezewa muda kidogo kutokana na kukabidhiwa ujenzi mwengine  kama vile Choo , ukarabati wa Ofisi ya Kata pamoja na nyumba ya walinzi tunasubiria majibu lakini kwa ujenzi wa Stendi tunakimbizana ili mradi huu ukamilke kwa wakati kama tulivyokubaliana" Amesema Eng. Yassini.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.