MKURUGENZI MANISPAA MOROGORO ATOA NENO LA SHUKRANI KWA LADIESTALK TANZANIA KUTAMBUA MCHANGO WAKE.
Cheti cha Pongezi Kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Joyce Mugambi,akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye pia ni mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Jafari Makupula.
MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ametoa neno la shukrani kwa Taasisi ya Ladiestalk Tanzania baada ya kumzawadia Cheti cha Shukrani katika Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Taasisi hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea cheti cha shukrani , Lukuba,amesema kuwa Ladiestalk Tanzania , imefungua njia katika kuimarisha nguvu za Wanawake ndani na nje ya nchi kutokana na kuandaa na kusimamia Tamasha la Kuwakutanisha Wanawake liloandaliwa kwa ubunifu na ustadi huku likijumuisha zaidi ya Wanawake 120 .
Lukuba, ameuomba uongozi wa Ladiestalk Tanzania, kupitia Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Salome Sengo, kuhakikisha kwamba Kongamano hilo linakua endelevu ambapo amebainisha kwamba kuendelea kwa Kongamano hilo kila mwaka kutasaidia kukuza uwelewa na kujiamini kwa Wanawake katika Nyanja mbali mbali kiuchumi.
Naye Mkurugenzi wa Ladiestalk Tanzania, Salome Sengo, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, kwa jinsi anavyowatetea Watoto wakike hususani katika Suala la Elimu.
""Nampongeza sana Dada yangu Sheilla Lukuba, utendaji wake umetuonyesha njia sisi Wanawake, tunajifunza mengi kutoka kwake, Dada Jasiri na mwenye maamuzi, nyuma hatukuwa na Choo cha Mtoto wa Kike, lakini ujio wake tumeshuhudia Choo Cha Mtoto wa Kike Shule ya Sekondari Tubuyu kikizinduliwa hii ni heshima kwetu na wanawake Wote, kikubwa tutamuunga Mkono kwa kila jitihada ambazo anazifanya ndani ya Manispaa yetu ya Morogoro hususani katika Kuijenga Manispaa yetu na usimamizi bora wa Miradi"Amesema Sengo.
Amesema zoezi la Utoaji wa vyeti ni moja ya Shukrani kutoka kwa Taasisi ya Ladiestalk Tanzania kutokana na mchango wao mkubwa katika kufanikisha Kongamano hilo.
Taasisi ya Ladiestalk Tanzania, iliandaa Kongamano la Wanawake Julai 25,2020 ambalo lilijumuisha zaidi ya Wanawake 120 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Savoy Hotel Manispaa ya Morogoro.
Post a Comment