Header Ads

RC SANARE AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA MOROGORO NA KUSISITIZA MAPATO NA MATUMIZI YASOMWE KWA WANANCHI.

Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mhe Loata Sanare akizungumza na wananchi,  ,Katibu tawala Mkoa Morogoro,Mhandisi Emanuel Kalobelo (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Regina Chonjo pamoja na Meya Mnaispaa ya Morogoro, Mhe Pascal Kihanga (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, mhe. Regina Chonjo akizungumza na wananchi katika Shule ya Msingi Berhard Bendel

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, mhe. Regina Chonjo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bungodimwe.


Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mhe. Loata Sanare akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bungodimwe mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili 2 vya madarasa vilivyokamilika.




Bweni la wanafunzi wa Kiume Shule ya Msingi Berhard Bendel.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Shule ya Msingi  Berhard Bendel.


Wakuu wa Idara Manispaa ya Morogoro wakifuatilia makini ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Shule ya Msingi Berhard Bendel.
Mkuu wa Mkoa akiwa amemshika mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Berhard Bendel.

Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mhe Loata Sanare akizungumza na Wananchi katika eneo la mradi wa kivuko kinachounganisha Mtaa wa Kileka na Ofisi ya Kata.


Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro , Sheilla Lukuba akiwasalimia wananchi wa Kata ya Mlimani.
Diwani Kata ya Mlimani , Zinduna Kombo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bungodimwe wakisalimia Viongozi.


Madarasa yaliyo tengenezwa katika Shule ya Sekondari Bungodimwe.

Diwani wa Kata ya Mlimani , Mhe. Zinduna Kombo.



MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loata Sanare, amefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la kuboresha kasi ya uwajibikani na upatikanaji mzuri wa huduma kwa wananchi.

Ziara hiyo imeanza leo Februari 28 , 2020 katika Kata ya Mlimani ikiwa ni moja ya ziara zake ambazo analenga kuziifanya katika Kata zote 29 zilizopo Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, RC Sanare, ameanza ziara yake katika Shule ya Msingi  Berhard Bendel isiyo ya Serikali iliypo Kata ya Bigwa kufuatia maagizo aliyoyatoa katika Uongozi huo juu ya ukarabati wa miundombinu  ya Bweni la Wanafunzi wa Kiume wa shule hiyo.

Aidha, RC Sanare, baada ya ukaguzi huo wa bweni amejidhirisha kwamba maagizo aliyoyatoa yamefanyiwa kazi na sasa Bweni hilo lipo tayari kwa ajili ya matumizi kwa wanafunzi.

"Nipo hapa shuleni kwa ajili ya kuangalia nilichokiagiza, kwakweli hali haikuwa nzuri katika Bweni la wanafunzi hivyo katika kikao changu nilimuagiza Mwalimu Mkuu kuhakikisha yale mapungufu yaliyopo katika Bweni la wanafunzi wa Kiume yanafanyiwa kazi na sasa nimejiridhisha kwa macho yangu kwamba hakuna shida tena , napenda kusema sasa rasmi wanafunzi kulitumia bweni hilo lakini pale mnapoona kuna shida na manataka msaada wa Kiserikali msisite  kutuambia nasi tutawapatia ushirikiano  lengo ni kuboresha  elimu katika Shule zetu zilizopo katika Mkoa wetu wa Morogoro na umeniambia una shule nyengine usisite nitakuja kikubwa nenda kaweke mazingira vizuri "Amesema RC Sanare.

Pia amesema lengo la kufanya ziara katika shule binafsi ya Berhard Bendel ni kuhakikisha kwamba wana boresha miundombinu ili kuongeza viwango vya ufaulu kwani katika takwimu za viwango vya ufaulu katika ngazi za Mkoa  hawaangalii shule za Serikali pekee bali waangalia matokeo kwa ujumla katika Mkoa mzima.

Pia amemuagiza Mhandisi wa Mnaispaa ya Morogoro kusimamia majengo ya Shule kikamilifu kuanzia shule za Serikali pamoja na zile binafsi pamoja na kusisitisha ujenzi kwa kuweka alama ya X majengo yote ambayo yanajengwa bila ya vibali vya ujenzi.

Katika ukaguzi huowa maendeleo shuleni, hakuishia katika shule hiyo pekee bali amepata nafasi ya kutembelea Shule ya Sekondari Bungodimwe iliyopo Kata ya Mlimani na  kukagua Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa vilivyomalizika na kugharimu shilingi Milioni 25 na laki 9.

Amesema kuwa, kwa jinsi Ujenzi huo ulivyokamilika ameridhika na ujenzi huo na kusema thamani ya pesa imetumika huku akiwapongeza sana Wananchi kwa jitihada walizozionesha lakini amesema bado nguvu za Wananchi zinahitajika ili kuendelea kutanua miundombinu ya shule hiyo Ikiwamo ukarabati wa Madarasa, ujenzi wa Jengo la Utawala , Maabara pamoja na Ofisi ya Mkuu  wa Shule.

Pia amewataka TARURA ,  kuichonga barabara hiyo inayowaunganisha wananchi wa Towelo yenye urefu wa KM 3.5 kutoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Nduguzangu TARURA mliniambia kwamba mlishaipitia barabara hii katika Bajeti ya Mwaka 2020/2021 lakini mpaka leo sioni utekelezaji, sijaridhishwa na majibu yenu ya kupunguza bajeti kwahiyo hao viongozi wenu wa Makao Makuu wakija naomba nikutane nao na niwalete waone kama watapunguza aula laa, ombi langu ni kwamba iangalieni hii barabara kwa jicho la huruma ili kunusuru watoto zetu kuacha utoro, wanafunzi kufika kwa urahisi na wananchi pia kunufaika na huduma hii muhimu" Amesisitizia RC Sanare.

Pia amewataka Wanafunzi wasome kwa bidii na kuacha kucheza ili waweze kutimiza ndoto zao katika maisha na kuwa Viongozi bora wa Taifa ili kubadilisha maendeleo hususani watoto wa kike kwani viongozi wengi wa kike duniani ni kwamba wameaminiwa kulikana na elimu zao.

Pia RC Sanare,ameahidi kuchangia shilingi Milioni Moja pamoja na Mkuu wa Wilaya shilingi laki 5 kwa ajili ya uboreshaji wa maendeleo katika shule hiyo.

Amesema Wazazi Katika kata  hiyo ni wagumu kuchangia elimu lakini furaha yake ni kuona baada ya miaka 5 au 10 viongozi wa Morogoro wanapatikana katika Shule za Morogoro.

Katika hatua nyengine, amewataka Watendaji wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro kuanzia ngazi za Mitaa na Kata wawe na utaratibu wa kusoma mapato na matumizi katika viako vyao wanapokuatana na wananchi kwani suala hilo lipo kisheria na agenda kubwa ziwe ni kujadili ulinzi na usalama pamoja na mapato na matumizi kabla hawajaingia katika ajenda mpya.

Agizo hilo amelitoa kufuatia malalamiko ya wananchi katika kikao cha wazi kilichofanyika katika Ofisi ya Kata ya Mlimani huku baadhi ya wananchi wakilalamikia Uongozi wa Kata pamoja na Mitaa kutosoma mapato na matumizi jambo linalowapelekea kutokuwa na uelewano mzuri kati ya wananchi na viongozi wa kata hiyo.

Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina Chonjo, ameiomba TARURA kuwapatia njia nzuri ili magari yaweze kufikika katika Shule hiyo ili kurahisisha usafiri kwa Walimu na Wanafunzi pamoja na Wananchi wanaoitumia barabara hiyo japo sio kwa kiwango cha  lami lakini hata kuchonga sehemu korofi itasaidia.

"Barabara hii ni muhimu sana , hivyo mkiitengeneza vizuri itakuwa si mkombozi wa wanafuzni pekee bali hata kwa wananchi wanoitumia barabara hii watanufaika na huduma hii ya barabara , walimu watakuja shuleni, utoro kwa wanafunzi  utapungua kutokana na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Shule hii ya Bungodimwe,  na wakazi wa huku wataitumia kwa ajili ya kusafirisha bidhaa zao na kwenda pamoja na kurudi majumbani "Amesema DC Chonjo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, amempongeza Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kuwapatia fedha shule zote za Manispaa ya Morogoro kupitia mpango wa Elimu bure bila malipo pamoja na pesa za miradi ya maendeleo hususani miradi  ya kimkakati ,  Mkuu  wa mkoa Morogoro Mhe. Loata Sanare kwa  hatua za kuboresha maendeleo ya elimu  , Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo ya usimamizi mzuri wa miradi  na kazi kubwa na nzuri wanazozifanya ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha amepongeza  juhudi kubwa zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood kufuatia kutoa pesa nyingi za mfuko wa Jimbo pamoja na pesa zake binafsi katika kuchangia maendeleo ya Manispaa  ya Morogoro.

Naye Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro, mhe. Pascal Kihanga, amesema shule za Manispaa ya Morogoro zinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo amemuomba  Mkuu wa Mkoa kueleza na kuwapa maelekezo pale anapoona kuna makosa ili wajirekebishe kuliko kuyaacha na kuwagharimu baadae.

Kihanga, amewataka Wazazi kuendelea kuchangia pesa na vifaa mbalimbali ili kuleta maendeleo katika shule hiyo.









No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.