Header Ads

Meya Manispaa ya Morogoro awaasa Vijana Kuacha kulalamikia Ajira




Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro , Mhe. Pascal Kihanga.

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao.


Aidha, amesema  kwa sasa mambo yamebadilika sana hivyo watoe fikira za kumaliza chuo na wale waliopo mitaani  na kujiwekea fikra za kuajiliwa wakati wao wenyewe wanaouwezo wa kutengeneza ajira kutokana na mambo watakayobuni kufanya.

Amesema  kuwa kwa sasa vijana wanayonafasi ya kubuni miradi na serikali ikawasaidia kuiendeleza mbele kwa kuwapa mitaji ili waifanikishe.

"Vijana acheni Kulalamikia ajira, zama za mababu zetu ajira zilikuwa za kutosha ila kwa sasa kila mmoja akimaliza chuo au yule aliyopo mtaani anataka aje  apate ajira serikalini haiwezekani, hivyo nawaasa kujiwekea malengo ya kujiajiri wenyewe ili muingine katika soko la ushindani," amesema Mhe. Kihanga.

Pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu wa muda. “Muda ni kitu cha msingi na kukitunza sana,” amesema .
“Nilikuwa na ndoto ya kuja kuitumikia jamii, nilikataa kazi nyingi za kuajiriwa ili kuifuata ndoto yangu, nilikuwa naamini maisha yangu yapo kwenye siasa, mpaka sasa niliitambua njia yangu na ndio njia niliyopitia,” amesisitizia .

Katika hatua nyengine, amesema  kuzaliwa kwenye familia maskini hakumaanishi kuwa huwezi kujinasua na kuwa na maisha unayotaka.

“Usikasirike kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni kujiondoa katika umasikini,” ameongeza Mhe. Kihanga.

“Mungu kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika maisha yako, usifate mkumbo, fanya maamuzi sahihi kwa maisha yako ya baadae.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.