HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 15,587,438,373
Akiwasilisha bajeti hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi aliwashukuru Wah. Madiwani kwa ushirikiano na kazi nzuri. Pia alimshukuru Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe na Kamati yake ya Usalama (W), Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya na wataalamu wote kwa kazi nzuri.
Aidha, aliwashukuru viongozi wa CCM wakiongozwa na Mkt CCM (W) Ndg. Shaban Sajilo na Katibu CCM (W) Bi. Josephine Mbezi kwa usimamizi madhubuti wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015/2020.
Makisio hayo ya Bajeti 2020/2021 (Tshs. 15,587,438,371) yalisomwa kwenye Mkutano Maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Baraza limefanyika leo tarehe 18/2/2020 kwenye ukumbi wa kisasa wa Halmashauri.
Mwisho alisisitiza kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwani hali ya Halmashauri kifedha sio nzuri kabisa. Wataalamu wajieleze kwanini hawajakusanya mapato kama ilivyopitishwa kwenye bajeti ya 2019/2020.
Gairo Maendeleo Fasta kwa Mwendo Mdundo
Post a Comment