Header Ads

Afisa Mwandikishaji Jimbo la Ilala ataka zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura liendeshwe kwa kuzingatia sheria na kanuni za TUME.



Afisa Mwandikishaji  Jimbo la Ilala, Jumanne Shauri akifafanua jambo.

AFISA Mwandikishaji wa Jimbo la Ilala, Jumanne Shauri,  amewataka BVR Operators na Waandikishaji wasaidizi    kuendesha  zoezi hilo kwa mujibu wa Sheria , Kanuni pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ameyazungumza hayo, wakati wa Ufunguzi wa Uandikishaji ulioanza leo Wilaya ya Ilala tarehe 14 hadi tarehe 20 Februari 2020.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amewapongeza washiriki wote walioteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi hilo muhimu la Uandikishaji wa Wapiga kura.

"Matumani yangu zoezi hili litaenda vizuri kulingana na mafunzo na elimu ya kutosha  waliyoipata  waandikishaji  ili kutekeleza wajibu na majukumu yao  katika kufanikisha zoezi hili muhimu, pia nahakika baadhi waandikishaji walibahatika  katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kwa mara ya kwanza katika mfumo huu wa sasa wa Teknolojia ya BVR (Biometric Voters' Registration) mwaka 2015 hivyo wana  uzoefu katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa zoezi hili" Amesema Shauri.
Aidha, amewataka wanamafunzo wale waliopata ujuzi kipindi cha nyuma na wale wapya kushirikina na wa kutumia uzoefu walionao kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa , kwa bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo na kuwafundisha wenzao ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi lililopita ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Pia amewaambia kwamba Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura na watazamaji watazamaji wakati wa zoezi zima la uboreshaji ambao watapatiwa vibali maalum ambavyo vitawaruhusu kuingia katika vituo vya kuandikisha jambo ambalo ni muhimu na litasaidia kuleta uwazi katika zoezi hilo.
"Lazima mtambue kwamba , Mawakala wa Vyama Vya Siasana Watazamaji hawatakiwi kuwaingilia watendaji mnapotekeleza wajibu wenu, hivyo maelekezo zaidi kuhusu suala hili yapo kwenye vitabu vya maelekezo mlivyopatiwa na ni muhimu kuyazingatia ili zoezi letu lifanyike kwa mujibu wa Sheria , kanuni na maelekezo" Ameongeza Shauri.

Mbali  na melekezo, amewaambia kuteuliwa kwao kumetokana na kuaminiwa hivyo wanauwezo wa kufanya kazi hiyo, kikubwa ni kujiamini na kujitambua na kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume ili waweze kufanya kazi wakati wa zoezi la Uandikishaji  pamoja na kufuata Sheria , kanuni, maelekezo na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala , imedhamiria kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kuwataka watendaji kuhakikisha wanayajua na kuyatambua vyema maeneo watakayofanyia kazi ikiwemo miundombinu ya kufikia katika Kata na Vituo.

Hata hivyo amechukua nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutekeleza haki zao za msingi za kikatiba na hatimaye kwenda kuwachagua Viongozi watakao weza kuwaletea maendeleo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa Diwani, Mbunge na Rais.




No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.