Header Ads

Breaking News: Mkutano Maalum wa Bajeti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ukiendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa leo Februari 12, 2020.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba,  akifungua mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga kusoma hotuba ya kuwasilisha rasmi Bajeti ya mwaka 2020/2021 katika mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa leo Februari 12, 2020.

Mbunge Viti Maalum, Mhe. Christine Gabriel Ishengoma, akitoa pongezi kwa Manispaa ya Morogoro kutokana na wasilisho zuri la Bajeti ambayo watakwenda kuipitia Bungeni.(kushoto) Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Komanya Spear Aman, (katikati), Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana.


Naibu Meya Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mhe. Sengo Isihaka (kulia) , Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro (katikati) na Diwani wa Kata ya Mazimbu , Mhe. Pascal Kihanga, (kushoto), Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogro, Sheilla Lukuba, wakifuatilia kwa makini taarifa za wasilisho la Bajeti katika mkutano .

Wahudhuriaji wa Mkutano wakifuatilia kwa makini wasilisho la Bajeti.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Sengo Isihaka wakionekana na furaha kabisa leo katika wasilisho la Bajeti ya Manispaa. 


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga (kushoto), akifungua dua kabla ya mkutano kuanza, (kulia) Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Sengo Isihaka .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini, Ndg. Fikiri Juma akifuatilia kwa makini wasilisho la Bajeti ya Manispaa leo.


 Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Komanya Spear Aman, (kushoto), akiwa pamoja na (katikati), Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana na Mbunge Viti Maalum, Mhe. Christine Gabriel Ishengoma wakifuatilia kwa makini wasilisho la Bajeti ya Manispaa leo.
Waheshimiwa Madiwani wakishauriana jambo katika wasilisho la Bajeti ya Manispaa.
Waheshimiwa Madiwani wakishauriana jambo katika wasilisho la Bajeti ya Manispaa



Afisa Utumishi Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo pamoja na ,mwandaaji wa mikutano wakisikiliza kwa makini wasilisho la bajeti.

Wakuu wa Idara Manispaa ya Morogoro wakisikiliza kwa makini wasilisho la Bajeti.

Mhe. Diwani wa Kata ya Boma, Amiri Juma Nondo, akitoa mapendekezo katika mkutano huo.


Mchumi wa Manispaa ya Morogoro, Rubeni Urasa (kushoto) , akielezea mipango ya Bajeti ya Manispaa ya Morogoro.(kulia) Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, Waziri Kombo akipitia taarifa.
Mkutano huo bado unaendelea Taarifa zaidi tutazitoa baada ya kumalizika kwa kikao , lakini kubwa zaidi ni utekelezaji wa miradi mikubwa minne ya Sekta ya uchumi na uwekezaji ikiwamo Mradi wa Soko kuu la Kisasa, Mradi wa Ujenzi wa DDC, Mradi wa Stendi ya Daladala Mafiga pamoja na Mradi wa Stendi ya Kaloleni.

Pia wasilisho hilo limegusia Sekta ya Ardhi, Sekta ya Elimu (msingi na Sekondari), Miundombinu, ujenzi wa maabara za Sayansi, Sekta ya Afya, Sekta ya Mazingira, Utawala bora, Sekta ya Maendeleo ya Ustawi wa Jamii na Vijana, Hali ya Maambukizi ya VVU Katika Manispaa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2019, Mwenendo wa ukusanyaji wa mapato , Sekta ya Ujenzi, Sekta ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika nk.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.