Header Ads

AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA MOROGORO MJINI AFURAHISHWA NA UTULIVU WA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA





 Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, akiwa na Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo Morogoro Mjini, Waziri Kombo katika kuangalia zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura leo asubuhi katika kituo cha Kata ya Kihonda.


Afisa Mwandikishaji jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, amefurahishwa na utulivu unaoendelea katika zoezi zima la Uboreshaji Daftari la Kudumu la wapiga kura lililoanza leo Februari 3 hadi 9 mwaka huu 2020 katika Manispaa ya Morogoro.
Afisa Mwandikishaji Msaidizi  wa Jimbo la Morogoro, Waziri Kombo akifuatilia zoezi hilo leo.
Afisa Mwandikishaji jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba akizungumza na wananchi waliojitokeza katika kituo cha uandikishaji Mkundi leo asubuhi.

Mwandikishaji Msaidizi akiwa kazini.
BVR Operator akiendelea na hatua za uandikishaji.
Baadhi ya Vitambulisho vilivyofanyiwa majaribio ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  mwaka jana 2019, mwezi machi katika Kata ya Kihonda ambapo havitatumika hivyo wakazi wa Kihonda wameshauriwa wakajiandikishe upya.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Sheilla , amesema utulivu unaoendelea ni kiashiria tosha cha kwamba zoezi hilo litamalizika vizuri.
Baadhi ya Wananchi wakiwa katika foleni leo asubuhi katika Kituo cha Uandikishaji Mkundi.
Amesema kuchaguliwa kwao kumetokana na kuaminiwa na hivyo wanapaswa kutambua uzito na umuhimu wa zoezi hilo na kuwataka watekeleze zoezi hilo kikamilifu.
Aidha,amechukua nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutekeleza haki zao za msingi za kikatiba na hatimaye kwenda kuwachagua Viongozi watakao weza kuwaletea maendeleo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa Diwani, Mbunge na Rais.

Aidha amesema kuwa katika  zoezi hilo, wataandikishwa wapiga kura wapya, kwa maana ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha mwaka 2015, ambao wametimiza miaka 18 au watakao kuwa na umri wa miaka 18 ifikapo 2020, pia watapatiwa vitambulisho vipya kwa waliopoteza au kuharibika vitambulisho vya awali na watafutwa kwenye Daftari wale ambao wamepoteza sifa za kuwa wapiga Kura.
"Kikubwa ninachowaomba Waandikishaji kwamba wakati zoezi hili likiendelea hakikisheni mnakuwa  karibu na wananchi wakati wa zoezi hili ili kumfanya aweze kutoa taarifa zilizosahihi za mpiga Kura na kuziingiza katika mfumo." Amesema Sheilla.
Katika hatua nyengine, amewataka Wenyeviti wa Mitaa,  Maafisa Watendaji wa Mitaa na Kata pamoja na Wananchi kwa ujumla kuhamasishana ili watu wote wenye sifa waweze kuandikishwa na kupata haki zao za kikatiba katika kushiriki chaguzi zijazo.
Naye,  Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Jimbo la uchaguzi la Morogoro, Waziri Kombo,amewataka waandikishaji hao kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kutekeleza zoezi hilo kwa  kwa umakini na ufanisi pamoja na  utunzaji wa vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.
Amesema matarajio yake ni kuona  zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura linafanikiwa kwa kiwango kikubwa ili kuwa na taarifa sahihi za wapiga Kura.
Pia amesisitizia umuhimu wa kuzingatia umakini katika maeneo yao ya kazi ikiwemo usambazaji wa vifaa na ufunguaji na ufungaji wa vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa wakati uliopangwa.
Hata hivyo amewaambia wasisite kuwasiliana na Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Morogoro kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao.
"Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Afisa mwandikishaji Jimbo la Morogoro imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na hivyo nanyi mna kazi ya kuhakikisha kuwa mnatekeleza kikamilifu kwa upande wenu" amesema Kombo.
Mwisho amewataka waandikishaji kutekeleza majukumu yao waliyopewa kwa umakini, uaminifu, uadilifu na uweledi wa hali ya juu.
Kwa upande wa Mwananchi, Shafii Juma Fundi, amesema zoezi hilo ni zuri huku akiwasihi  wananchi wenzake kujitokeza kwa wingi ili kupunguza usumbufu wakati zoezi hilo litakapoelekea mwishoni.






No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.