Header Ads

Afisa Uandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini atoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.





Afisa Mwandikishaji Jimbo la Morogoro Mjini, Sheilla Lukuba, akionyesha kadi yake mara baada ya kujiandikisha leo.





Akizungumza katika kituo Cha Uandikishaji Nguzo Kata ya Boma, amesema kuwa amefarijika kuona  wananchi wamehamasika na zoezi Hilo.

Aidha, Sheilla,  amesisitiza kuwa zimebaki siku 4 tu zoezi la uandikishaji likamilikeJimboni humo, hivyo wananchi wenye sifa wajitokeze kujiandikisha na kupata vitambulisho vya mpiga kura.

Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura Jimbo la Morogoro Mjini ,lilianza   tarehe 03/02/2020 na litakamilia tarehe 09/02/2020.

Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmsahuri ya Manispaa ya Morogoro, limeanza rasmi huku wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi Hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika maeneo tofauti.

Aidha aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Hata hivyo, amewataka  wananchi wajitokeze kwa wingi ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Manispaa ya Morogoro limeanza rasmi na linatarajia kumalizika jumapili wiki hii Februari 9, 2020.



No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.