MANISPAA MOROGORO YAZINDUA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA UHAMISHO WA WANAFUNZI KWA NJIA YA MTANDAO.
Afisa Elimu Taaluma Manispa ya Morogoro , Jaribu Malambughi akitoa taarifa ya mafunzo. |
Walimu wakuu shule za Serikali , Binafsi pamoja na walimu wa TEHAMA wakiendelea na mafunzo mfumo mpya wa uhamisho wa wanafunzo kwa mtandao leo. |
Taarifa ya Mafunzo hayo imetolewa na Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Morogoro , Jaribu Malambughi katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa leoFebruali 19,2020 .
Akizungumza na Waandishi wa habari, Malambughi, amesema kuwa faida za mfumo huo ni pamoja na kurahisisha kazi, kupata takwimu kwa haraka na kurahisisha mipango ya maendeleo shuleni pamoja na kujua hali ya mdondoko (utoro) kwa wanafunzi.
"Ndugu wakuu wa shule , walimu wa TEHAMA/TAALUMA /MAKAMU mpo hapa kwa ajili ya kupata mafunzo juu ya mfumo mpya wa usajili na uhamishaji wanafunzi kwa njia ya mtandao, hivyo matumani yangu baada ya mafunzo haya kazi itafanyika vizuri na hatutegemei kupata malalamiko yoyote kuhusu mfumo huu wa kisasa ambao unalengo la kurahisisha kazi, kwahiyo tunajifunza kwa nadharia na vitendo ili tuelewe mfumo huu vizuri" Amesema Malambughi.
Aidha, amesema mfumo huo unaojulikana kwa jina la Prems umetokana na maagizo ya barua ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ya mwaka 2018 ambayo iliagiza wanafunzi wote walipo katika shule binafsi na za Serikali kuwa katika TSM.
Pia amesema mfumo huo utasaidia Maafisa elimu wa Manispaa kuweza kupandisha taarifa za wanafunzi kutoka shule, kupokea na kuidhinisha uhamisho wa wanafunzi pamoja na kuhariri taarifa zote za uhamisho.
Katika hatua nyengine, amesema kuwa mfumo huo utakuwa umegawanyika katika majukumu ya walimu Wakuu wa pande zote mbili ikiwemo wa Shule binafsi pamoja na Shule za Serikali.
Miongoni mwa kazi kwa upande wa Wakuu wa Shule za Serikali ni pamoja na kupokea na kuhakiki taarifa za wanafunzi kwa TSMS9 zao, kutuma, kupokea na kukubali maombi ya uhamisho pamoja na kusimamia usajili wa kidato cha kwanza kwa kuwapa namba ya usajili.
Katika kuhitimisha hilo, amesema kwa Wakuu wa shule binafsi mfumo huo utawasaidia kupakua templeti katika mfumo ambapo template hizo zitakuwa katika makundi ya umoja na wingi kwa ummoja itaruhusu kusajili mwanafunzi mmoja mmoja atakayefika baada ya wanafunzi wa pamoja kufanyiwa usajili.
Pia amesema katika usajili huo wa mfumo mpya , walimu wakuu hawaruhusiwi kusajili wanafunzi ambao hawajawasili shule kwa ajili ya masomo bali utasajili wale ambao wamewasili ndio watakao patiwa usajili ili kuepusha usumbufu kwa wazazi baada ya kubaini kwamba mwanafunzi amepelekwa shule binafsi itamlazimu mzazi aanze upya kufuatilia uhamisho.
Ameseisitiza suala la uhamisho ni lazima mzazi apewe Prem namba kutoka shule ambayo mwanafunzi anasoma ili kuweza kumruhusu kutafuta shule lakini prem namba hiyo katika mfumo wa uhamisho wa mtandao itadumu kwa muda wa siku 14 baada ya kupita kama mwanafunzi hajafanikiwa kupata shule itamlazimu mzazi kuanza upya maombi.
Mafunzo hayo yataendelea Tarehe 20, 2020 kwa walimu wakuu wa Shule za Msingi Serikali pamoja na Shule binafsi.
Post a Comment