Waziri Zungu apiga marufuku uingizwaji wa mifuko mbadala ambayo haijakidhi viwango, msako kufanywa nchi nzima
WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Zungu amepiga marufuku uingizwaji na utengenezaji wa mifuko mbadala ambayo haijakidhi viwango vilivyowekwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Agizo hilo alilitoa jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.
Aidha alisema msako mkali utafanywa nchi nzima kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wasambazaji na watengenezaji wa bidhaa hizo zisizo na viwango.
Waziri Zungu alisema licha ya kuingiza mifuko hiyo kwa njia za magendo, ubora wa bidhaa hizo umekuwa ni hafifu na usiokidhi vigezo vilivyowekwa ili kuyafanya mazingira yawe salama.
Post a Comment