Header Ads

Chombohuru kinatoa Pongezi kwa Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Bariadi



Aliyekuwa Afisa Tarafa wa Ukonga Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam na sasa Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Bariadi, Ndg. Nicodemus Shirima (wapili kutoka kushoto)aliyeshika Mic wakati wa moja ya ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema.
BODI  ya Wakurugenzi Chombohuru Media kinapenda kuchukua nafasi hii kwa ajili ya kumpongeza aliyekuwa Afisa Tarafa wa Ukonga, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam, Ndg. Nicodemus M. Shirima kwa kupata uteuzi wa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya BariadiMkoani Simiyu.

Aidha , Chombohuru Media kinampongeza  na kumtakia kila la kheri Ndg. Nicodemus Shirima,  katika majumkumu yake mapya ya Katibu Tawala Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.

Wiki iliyopita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (mst) George H. Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa kwa mujibu wa Sheria alifanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya nane(8) kwa kuwapandisha vyeo Makatibu Tarafa na kuwabadilisha vituo vya kazi Makatibu Tawla watatu (3).

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.