Header Ads

TANGAZO KWA UMMA KUHUSU WALIOUZIWA VIWANJA MANISPAA YA MOROGORO



MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro anawatangazia Wananchi wote walionunua Viwanja Manispaa katika miradi mbali mbali ya Viwanja vilivyopimwa kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa wajisalimishe mapema

Miongoni mwa wadaiwa wanaoguswa ni pamoja na 


  1. Wasiolipa kabisa
  2. Waliolipa kidogo  pamoja na 
  3. wale waliobakiza malipo kidogo 
Manispaa imeongeza muda wa kulipa madeni hayo ndani ya Siku Thelasini (30) kuanzia tarehe 01/12/2019 mpka Desemba 31, 2019.

Kwa wale wote watakao shindwa kulipa; Viwanja vyao vitauzwa tena kwa njia ya mnada

Lipa sasa kuepusha usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza. Kwa taarifa zaidi fika Ofisi za Ardhi Manispaa ya Morogoro Chumba namba 8 na 9 au wasiliana kwa namba za simu 0755685592/0653216239

Tangazo hili limetolewa  na ,

                                        Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
                                                   Sheilla Edward Lukuba.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.