Header Ads

Mbunge Jimbo Morogoro Mjini akabidhi Vifaa vya Kuoshea Magari (Pump Machine) kwa Madereva wa Serikali Mkoa wa Morogoro vyenye thamani ya Shilingi Milioni 3,500,000/=.


Mhe. Abood (kulia) akikabidhi Pampu ya kuvutia maji na vifaa vyake kwa Chama Cha Madereva wa Serikali Mkoa wa Morogoro  vyenye thamani ya Shilingi Milioni 3 laki tano, (katikati) Mwenyekiti wa Chama hicho , Ndg. Zuberi Mustapha, (kushoto), Katibu wa Chama hicho , Ndg. Vicent Scott na nyuma ni Madereva waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano. PICHA Idara ya Habari Manispaa Morogoro.
Kamati Kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Mbunge wa Morogoro, Mjini, Mhe. Abood ikiwa imekaa tayari kuanza kwa kikao.

Mwenyekiti Chama Cha Madereva (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Mbunge Abood, Ndg. Ismail Hamadi.


Mhe. Abdulaziz Abood Mbunge Morogoro Mjini, akiandika dondoo wakati wa kikao cha Madereva kikendelea.

Katibu wa Chama cha Madereva , Ndg. Vicent Scott, akisoma taarifa kwa Mhe. Abood mara baada ya kikao hicho kufunguliwa,



Mbunge Jimbo Morogoro Mjini akabidhi Vifaa vya Kuoshea Magari (Pump Machine)  kwa Madereva wa Serikali Mkoa wa Morogoro vyenye thamni ya Shilingi Milioni 3,500,000/=. 

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amekabidhi Vifaa vya Kuoshea Magari Chama Cha Madereva wa Serikali Mkoa wa Morogoro  vyenye thamani ya Shilingi Milioni 3 laki tano

Hafla hiyo fupi  ya Makabidhiano imefanyika leo Desemba 28, 2019 kwenye Ukumbi wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, huku madereva kutoka Halmshauri mbali mbali wakijumuika katika kikao cha kawaida cha kikatiba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mhe. Abood, amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli inafanya kazi kubwa sana ya kuwatumikia Wananchi, hivyo wao kama watekelezaji wa Ilani wanawajibu wa kumsaidia Mhe. Rais kufikia malengo kwa kujitoa kwa Wananchi na kumpongeza kwa kazi nzuri anazozifanya kwa Maendeleo ya Tanzania hususani katika kufikia Uchumi wa Kati na Tanzania ya Viwanda.

Amechukua nafasi ya kuwapongeza Viongozi wa Chama hicho kwa kubuni wazo ambalo litawasaidia Madereva  wengi na kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili Madereva.
Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa Chama hicho kutaondoa dhana ya malalamiko ya kwamba Madereva wa Serikali ndio wanaongoza kuvunja Sheria za Barabarani na wasumbufu.

Kikubwa amewataka Madereva hao wawe waaminifu katika ufanyaji kazi wao kwani wamebeba siri za Viongozi wanaowaendesha.

Amesema kitendo cha kuwa na miradi kitawasaidia katika njia nyengine ya kuwaongezea kipato na kuendesha maisha yao kuliko kusubiria mishahara na kushauri kwamba mara baada ya miradi yao wanayoitaka kuanzisha kukamilika iwe na tija kwao na sio kugeuka kuwa mwanzo wa mafarakano na kuvunjika kwa miradi hiyo.

Katika hatua nyengine, amekiomba chama hicho kizingatie usawa na kuwaongeza wanawake ili kuonesha kwamba wakina Mama wanaweza.

Kikubwa zaidi amewataka Viongozi wa Chama hicho kuhakikisha wanakuwa wabunifu na waaminifu katika usimamizi mzuri wa rasilimazi za chama na kusimamia vyema mapato yanayotokana na miradi ili kujenga imani na Wanachama.

"Nawapa Mshine ya Cra Wash kubwa ili mradi wenu uanze, mimi si Mbunge wa maneno mengi, matumaini yangu mara baada ya mradi kuanza mtaongeza kipato chenu na kujikimu na maisha badala ya kusubiria mshahara" Amesema Mhe. Abood.

Naye, Mwenyekiti wa Chama hicho, Ndg. Zuberi Mustapha, ambeye ni Dereva wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, amemshukuru Mhe. Abood kwa kuwa nae katika kikao chao na kuwapongeza wanachama wote waliofika katika kikao.

Amesema lengo kubwa la kuunda Umoja huo ni kuweza kusaidia Serikali kupunguza ajali kwa kuwa  walimu wa wenzao amabo hawajapata mafunzo ya utumiaji sahihi wa barabara au kutojua Sheria za usalama barabarani.

Amesema wanataka kuhakikisha wanapunguza mlundikano wa wa Askari barabarani ambapo kwa sasa Jeshi la Polisi Usalama barabarani wanatumia idadi kubwa ya skari kuwapanga kila kona mfano mkoa wa Morogoro kwenda Dar Es Salaam, jambo ambalo linaongeza bajeti kubwa kwa Jeshi hilo hivyo kama shereia zitafuatwa wataipunguzia Bajeti Serikali kwa kupunguza ajali.

Amechukua nafasi ya Kuwapongeza Viongozi wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, ikiwamo Mhe. Abood, Mkuu wa Wilaya, mstahiki Meya, Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Baraza la Madiwani kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa Soko kuu la Kisasa, Stendi Mpya ya kisasa ya Msamvu, Ujenzi wa Stendi Mpya ya Daladala uliopo Kata ya Mafiga.

Amemuomba Mhe. Abood kuwafikishia salamu kwa Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo kwa kuwa mtetezi mkuu wa kada za madereva kwa kubadilishiwa kuingia katika muundo mpya wa kada ya Madereva kwa maelekezo aliyoyatoa kwa Wakurugenzi nchi nzima.
"Nimpongeze Mhe. Jaffo tunashukuru wote tumebadilishwa kwenda muundo mpya , ila tunamuomba atusaidie kupandishwa madaraja kwa wakati kwa madereva wenye sifa , tunamuombea 2020 ikimpendeza mwenye mamlaka ya uteuzi aendelee kumpatia wizara hiyo kwa mara nyengine tena" Amesema Zuberi

Hata hivyo, Katibu wa Chama hicho, Vicent Scott, ambeye ni Dereva wa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro, amesema tangia kuanzishwa kwa chama hicho mwaka Tarehe 20 Mei, 2018, mpaka sasa wanajumla ya wanachama 73 na jitihada za kuongeza wengine zinaendelea kufanyika.

Licha ya hapo amesema chama hicho kimekuwa kikikabiriwa na changamoto kama vile kukosa mfuko wa kuendeshea chama, ukosefu wa Vifaa tenki la maji lenye ujazo wa Lita 6000, mashine ya presha ya maji ambapo Mhe. Abood alianza na Pampu ili waendele na mradi, pamoja na kukosa fedha za kujengea mradi wao ambapo unahitaji shilingi Milioni 10 na tayari wameshakusanya Milioni 4 huku milioni 1 wakisaidiwa na bunge wa Gairo, Mhe. Shabibi.

Mbali na changamoto ,amesema matarajio yao kwa sasa ni pamoja na kukitangaza chama, kuhamasisha ongezeko la wanachama pamoja na kuwa na miradi mbalimbali.


No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.