Header Ads

Mkurugenzi Manispaa Morogoro awataka Vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo iliyotengwa na Manispaa



MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo iliyotengwa kwenye halmashauri zao huku akiwapongeza Wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo hiyo.
Aidha amesema kuwa wale wanaohitaji mikopo na elimu jinsi ya kuitumia ni vyema wakafika katika ofisi za Manispaa ya Morogoro  watapewa wataalamu wa kuwafundisha huku akisisitiza kuwa wanaochukua mikopo hiyo warejeshe kwa wakti ili na wengine waweze kupata.

" Halmashauri yetu ya Manispaa ya Morogoro tunatenga kila mwezi asilimia 10 ya mapato yetu kwa ajili ya kutoa mikopo kwa Vijana, Wakina Mama na Watu wenye ulemavu , hivyo nawomba Vijana wachangamkie fursa hiyo kwani kuwaacha Wakina Mama wakipata mikopo hiyo huku wao wakizubaa ni kushindwa kupiga hatua katika kuelekea Tanzania ya Viwanda"" Amesema Sheilla.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.