Header Ads

SERIKALI ITAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA NCHINI-WAZIRI KAIRUKI.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Uwekezaji  Angellah Kairuki akizungumza na Wafanyabishara na Wawekezaji.

SERIKALIya  Awamu ya Tano itaendelea  kutatua changamoto zawawekezaji na wafanyabiashara nchini, kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu nawadau mbalimbali kufanya mapitio ya Sera na Sheria ya Uwekezaji kwa lengo lakuboresha mazingira ya kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Uwekezaji  Angellah Kairuki alisema hayo  jana katika hotubayake katika  mkutano wa  Mashauriano kati ya Serikali ,Wafanyabiashara na Wawekezaji mkoani Morogoro uliofanyika mjini hapa.
Waziri Kairuki alisema ,jukumu la msingi la Serikalini  kuhakikisha kwamba sekta binafsi inawezeshwa kufanya biashara nakuwekeza katika mazingira ambayo ni wezeshi na yatakayopelekea biashara nauwekezaji wao kuzalisha kwa gharama nafuu na kuuza bidhaa zao kwa bei yaushindani.
Alisema , Serikali kupitia Ofisi ya Wazirimkuu  (Uwekezaji) inajiandaa   kuja na Sheria mpyaitakayoitwa Sheria ya Uwezeshaji wa Biashara (Business Facilitation Act) ambayokimsingi ndiyo itafanya utekelezaji wa yote ambayo yameelekezwa katikaBlueprint. 
Waziri Kairuki alisema, pia tayari Serikali imechukua hatua zakupunguza utitiri wa kodi, tozo na ada ambazo kwa muda mrefu zilikuwa kero kwawafanyabiashara na wawekezaji.
Alisema , kupitia  Bunge la Bajeti la mwaka 2018/2019na 2019/2020 zimefutwa takribani kodi, tozo na ada mbalimbali zipatazo163  na nyingine zilipunguzwa viwango vyake.
“ Kufuatia mabadiliko haya  sasa wawekezaji nawafanyabiashara wataweza kuokoa gharama na muda wa kutembelea ofisi mbalimbaliza uthibiti kwa ajili ya kupata vibali.  
Waziri huyo alisema , kutokana na mkakati huokutakuwepo  na uzalishaji wenye tija hata ukuaji wa uchumi wa Nchiutaongezeka na hivyo kuongeza fursa za ajira hususani kwa makundi ya wakinamamana vijana. 
Nao Wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika mkutanowa Mashauriano ulioongozwa na Mawaziri  10 miongoni mwao nane niManaibu Mawaziri kwa nyakati tofauti  wameeleza kuwa kinachowakwamisha katika shughuli zao ni Utitili wa Kodi unaosababishwa na Mfumo usiorafiki kwa taasisi za serikali zilizopewa jukumu la kukusanya Kodi.
Mkutano huo wa siku moja ulihudhuriwa na wadau na viongoziwa  ndani na nje ya mkoa wa Morogoro,wakiwemi viongoziwa  serikali wa wizara  mbalimbali na watendaji ngazi zamikoa, wilaya na Halmashauri.
Wafanyabiashara hao wanasema pamoja na dhamira ya serikalikutaka kufikia uchumi wa kati kwa uwekezaji wa viwanda, kinacho wakwamishakuendana na sera hiyo ni mfumo wa Kodi unaowafanya kushindwa  hatakufikia  malengo yao.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania ,Ally Mamba, alisema kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya Sheria natozo  zinawakandamiza na kushindwa kujiongeza katika biashara zao.
Mambo alisema,pamoja na kufanyika kwa vikao na baadhi yahalmashauri katika Suala la service levy,lengo ni jema la kuhakikisha Serikaliinapata mapato na wafanyabishara wanaendelea kufanya biashara na wamekuwahawatoi maelezo ya kutosha Jambo linalowakatisha tamaa kuendelea kufanyaUwekezaji.
Naye Mwakilishi wa wafanyabishara wa Mahoteli Mittah Muriaalisema bado suala la hoteli levy limekuwa likiwakandamiza wakati bado wanalipaVAT na kwamba hiyo Kodi ya namna ya ukokotoaii imekuwa haina maelezo ya kutoshampaka Sasa..
"Kodi ya hoteli levy bado si rafiki kwa mfanyabiashara natunaomba iangaliwe,"alisema Muria.
Wafanyabiashara wadogo Machinga, wakaomba vitambulisho vya awamuya pili vya Rais pamoja na kuwajari na kuwatambua viwe na picha kwa kilamfanyabiashara.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo Faustine France alisema,kumekuwa na changamoto ya wafanyabishara kupeana kitambulisho kutokana nakutokuwa na picha,huku wakaomba kutengewa maeneo ya kudumu yawafanyabiashara,ili waweze kufanya biashara bila tatizo.

No comments

Theme images by A330Pilot. Powered by Blogger.